Liko Katika Shirikisho la: .......................................Halmashauri Kuu ya Kanisa La Mungu

Headquarters, Dar es Salaam Tanzania, East Africa

Mchungaji: Jerome Chembe

HIVI NDIVYO TUNAVYOAMINI.

Tunaamini katika Mungu mmoja wapekee na aliye hai, Mwuumba wa mbingu na nchi; Ambaye Yesu Kristo ndiye Mwana wake wa pekee, aishiye tangu kuzaliwa kwake, akateswa kwa ajili ya makosa ya dhambi zetu, akazikwa, na akafufuka siku ya tatu ili kwamba sisi tuhesabiwe haki ya kuweza kuketi mkono wa Mungu, ambaye ni Baba yake yeye na sisi.

Tunaamini kuhusu kulala kwao walio katika wafu, kufufuliwa kwao wakati wa kurudi kwake Kristo mara ya pili, kubadilishwa kwa miili ya wakio hai, na hukumu ya wote wenye mwili.

Tunaamini juu ya toba, ubatizo wa kuzamisha kwenye maji mengi kwa ajili ya ondoleo la dhambi, maisha matakatifu, ushirikiano wa Wakristo na kwamba Bibia ni Neno lililovuviwa la Mungu.

C.F. Pryor