PASAKA

Aprili, 19, 2008, saa 12:00 Jioni—Aprili 20, saa 12:00 Jioni

Na James Herschel Lyda

Kutoka 12:1 BWANA akanena na Musa, na Haruni katika nchi ya Misri akawaambia, 2 Mezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu

Kumbukumbu la Torati 16:1 Na ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki;

 

Mwezi.

Tangu wakati wa kuanzishwa kwa Sheria za Musa, utaratibu wa kuhesa miezi uliojulikana kwa Wayahudi ulikuwa ni ule wa Miandanmo ya Mwezi lakini ilihusiana na mwelekeo wa machweo ya jua. Utaratibu wa mzunguko hadi kufikia siku za maadhimisho ya sikukuu za kidini ilitegemea sana na miandamo ya mwezi. Mwaka wa kidini ulianza katika kipindi kinachokaribiana na kile cha uski na mchana huwa na muda sawa katika mzunguko wa jua linapopita katikati ya mstari wa Ikweta (mwanzoni mwa majira ya baridi), yapata kama tarehe 21 Marchi. Utaratibu wa kuhesabu mwanzo wa mwezi ulianzia na mwandamo wa mwezi mpya. Kwa maneno mengine ni kwamba ulianzia katika maadhimiso ya mwandamo wa mwezi mpya kwa maneno mengine ni kwamba, mwaka ulianzia katika muandamo wa mwezi mpya uliofuatia mwanzo wa majira ya baridi. Kuna mambo yakupendeza kuyajua kuhusiana na hali hii. Inaonekana kwamba dunia iliumbwa katika kipindi hiki cha majira ya baridi wakti wa kipindi kile cha Uumbaji. Pia baada ya gharika kuu, Nuhu alifungua mlango wa Safina na kutoka kuanza maisha mapya kwenye Ulimwengu Mpya katika kipindi hiki cha baridi cha mwaka ule. Wana wa Israeli pia walitoka kutoka nchi ya utumwa ya Misri katika kipindi hiki hiki cha majira ya baridi. Kipindi hiki cha majira ya baridi ni cha kufanywa tena kwa mambo yote katika asili zake, ni ishara ya uumbaji mpya wa Mungu wa maisha mapya. Mwezi huu wa Abibu hatimaye ulijulikana kama mwezi wa Nisani.

Kutoka 12: 3Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkmwammbie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana koondoo kwa watu wa nyumba moja;

4na ikwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na atwae mwana kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yulr mwana kondoo.

5Mwana kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.

6 Nanyi mtamweka katika siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni

 

Kuanzia mwanzoni kabisa mwa uumbaji Mungu alitupa ishara ili kutufanya sisi tuitambue zawadi yake ya upatanisho ambayo ni huyu Mwana wake wa pekee Yesu Kristo. Katika uumbaji wake aliiumba mianga mikuu miwili ambyo ni Juan a Mwezi, ambavyo vinawakilisha Kristo na Kanisa. Aliviumba siku ya nne ya juma la uumbaji (2 Petro 3:8 inasema ….). Pia kwenye Pasaka yule Mwana Kondoo alitunzwa na kuhifadhiwa kwa muda wa siku nne. Katika siku ya miaka-elfu nne, Kristo na kanisa walizaliwa.

Kutoka 12: 7Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla.

Huu ni mfano wa mana ambayo kwayo Kristo alikufa. Taji la miiba na misumari aliyopigiliwa mikononi mwake, yote iluimchoma mwili wake na alkufa msalabani. Damu ilipakwa kwenye miimo ya milango kwenye hali sawa na ile damu iliyomwagika msalabani.

8Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chacu; tena pamoja na mboga zenye uchungu

 

Uchungu

Uchungu ni dalili ya mateso, kutendewa ukatili na utumwa kama tusomavyo Kutoka 1:14, Warumi 1:20 na Yeremia 9:15. Pasaka iliambatana na kula "mboga za uchungu", Kutoka 12:8, Hesabu 9:11. Hii mboga iliyoliwa hapa haijulikani ilikuwa ni ya aina gini. Huenda ilikuwa ni aina yoyote ya mboga chungu iliyopatikana mahali pale walipokuwa na iliyopatikana kipindi ambacho Paska ilikuwa inaadhimishwa. Mboga hii iliwakilisha taswira ya uchungu wa utumwa ambao kwao watu walitaabishwa kwao; na inachukuliwa pia kuwa ni taswira ya mateso ya Kristo.

9 Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani.

10 Wala msisaze kitu kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.

11 Te.mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya BWANA.

12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.

13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoingia nchi ya Misri.

14 Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele

21 Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo, mkamchinje pasaka.

22 Nanyi twaeni tawi la hisopo, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini, na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.

23 Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.

24 Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele.

25 Itakuwa, hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, BWANA atakayowapa, kama alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu

[Tunapaswa kuwa na meza iliyoandaliwa vizuri na sahani, bakuli na kikombe. Katikati ya meza tunakuwa na sahani ya nyama iliyopambwa kwa saladi Maridadi na figili zikiizunguka ile sahani lakini kukiwa tupu bila kuwepo nyama ndani yake. (Kama tungeweka nyama kwenye hii sahani, basi tungehukumiwa kwa kumsulibisha Kristo katika mwili kwa sababu yeye alikuwa ni ile sadaka kamilifu iliyokomesha aina zote za dhabihu). Tunaanza kwanza kwa kula zile mboga zenye uchungu (mchunga, ama aina yoyote ya mboga zenge uchungu za majani lakini zisizo na madhara zikiliwa) zichovywe kwenye maji ya chumvi huku tuliuliza maswali yafuatayo].

 

Je, Maswali ya Pasaka ni Yapi?

I. Je, ni kwa nini usiku huu ni wa tofauti na nyingine zote? Kutoka 12: 26 Kisha itakuwa hapo watoto wenu watakapowauliza, N’nini maana yake utumishi huu kwenu?

27 ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia

II. Je, ni kwa nini tunakula chakula hiki kisicho cha kawaida? Kutoka 1:13 Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; 14 wakafanya maisha yao kuwa machungu kwa kazi nguvu; kazi ya chokaa nay a matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba’ kwa kazi zao zote walizotumikishwa kwa ukali.

III. Je, ni kwa nini tunachovya mboga hizi yenye uchungu kwenye maji machungu? Ili kuyakumbuka machungu yaliyotokana na mateso ya utumwa ya Misri na jinsi walivyookolewa kwa kupitia Bahari ya Shamu Kutoka 1:14 wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa nay a matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.

IV. Je, yuko wapi Mwana kondoo wa Pasaka? Kwa kuwa sahani iko wazi. Mwana Kondoo wa Dhabihu amekwisha chinjwa tayari pale msalabani kwa hiyo teno la kuleta dhabihu kwenye sahani lingemaanisha ni kumsulibisha Kristo kwa upya. 1 Wakoritho 5:7 Basi, jisafisheni, mkate ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo mahkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; 8 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.

Waebrania 10:12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; 13 tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. 14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.

(Hatuli nyama kwenye ibada hii kwa sababu baada ya Kristo kusulibiwa ambaye ni "Ddhabihu Kamilifu", basi tutakosea kama tutamchinja mnyama tena. Hivyo basi tendo la sahani kuwa wazi inamaanisha kwamba Kristo ndiye Mwana Kondoo wetu wa Pasaka).

Kutoka 12:26 Kisha itakuwa hapo watoto wenu watakapowauliza, N’nini maana yake utumishi huu kwenu?

27 ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia

29 Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawapiga wazaliwa wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.

30 Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu.

31 Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, mkamtumikie BWANA kama mlivyosema.

32 Twaeni kondoo zenu na ng’ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi pia.

33 Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote. 34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabagani.

37 Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto.

38 Na kundi kubwa la watu waliochangamana nao wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng’ombe, wanyama wengi sana.

39 Nao wakaoka mikate isiyochachwa ya ule unga waliochukua walipotoka Misri, maana, haukutiwa chachu, kwa sababu walitolewa watoke Misri, wasiweze kukawia, nao walikuwa hawajajifanyia tayari chakula.

Tunauvunja na kuula mkate usiotiwa chachu huku tukinywa juisi ya zabibu. (Ni lazima iwe juisi ambayo haikutiwa aina yoyote ya amira au iliyochachishwa kwa kuwa chachu inawakilisha dhambi.) Wana wa Israeli waliamriwa kuondoa aina zote za chachu majumbani mwao kipindi hiki.

Kristo ambaye ndiye mfano wetu pia aliitunza sikukuu hii ya Pasaka.

Luka 22:7 Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka.

8 Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie Pasaka tupate kuila. 

9 Wakamwambia, Wataka tuandae wapi?

10 Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingine katika nyumba atakayoingia yeye.

11 Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba wageni, nipate kula Pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu?

12 Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo.

13 Wakaenda, wakaona kama walioambiwa, wakaiandaa pasaka.

14 Hata saa ilipofika, aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye.

15 Akawaambia, Nimetamani sana kuila Pasaka hii Pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu;

16 kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.

17 Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi;

18 Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja.

19 Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

20 Kikombe nacho baada ya kula; akasema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu,

Usiku wa Pasaka ulitolewa kwa Waisraeli miaka mingi sana kabla ya Kristo, lakini ilionyehsa kikamilifu usahihi wa mwezi na siku ambayo Kristo alipaswa kufa msalabani. Ilionyosha kwamba yeye alipaswa kuwa ndiye Mwana Kondoo wa Mungu asiye na dhambi wala waa lolote. Hii ni moja kati ya sikukuu ambazo tumeamriwa kuzitunza na kuziadhimisha milele.

Siku nyingine muhimu zimeorodheshwa kawnye vitabu vifuatavyo:

Kutika 20:8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;

10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.

11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa

Lakini Sabato ni lini? Sio Jumamosi kama wengine wanavyodhania. Pia sio Jumapili kama wengine wanavyoadhimisha. Lakini katika mwaka huu imetokea tu kwamba inaangukia siku ya Jumapil.Kwa mujibu wa mpango wa Mungu, mwezi wa kwanza unaanzia katika mwezi wa Abibu. Mwezi huu wa Abibu unaandama kwenye kipindi kilicho karibu na siku ambayo jua linapita katikati ya dunia kwenye mstari wa Ikweta, siku inayolingana masaa ya usiku na mchana (mwanzoni mwa majira ya baridi). Kwa mujibu wa utaratibu wa Mungu, huanza tarehe 18 Marchi, saa 12:00 jioni na huishia Marchi 19 jioni. Siku saba baada ya Marchi 25 inakuwa ni siku ya saba ya au Sabato. Hii hubadilika mwaka mmoja hadi mwingine kwa kuwa kalenda yetu haifuati utaratibu wa Mwandamo wa Mwezi.

Mwanzo 1:14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;

Lakini kalenda yetu mara nyingi huzingatia mwongozo wa jua ambalo wapagani huliabudu. Kwa mujibu wa matumizi ya kalenda tuliyonayo sasa ulimwenguni kote na ratiba za maisha yetu vinavyohusiana, inakonekana kuwa ni kama vigumu kuishi kwa kuitegemea kalenda hii Takatifu ya Mungu. Lakini siku moja inakuja ambayo kutatangazwa rasmi kuwa haya masaa hayana maana tena.

Warumi 14:5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa ni sawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.

6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.

REJEA KWENYE UKURASA MKUU