Kama uko tayari kuanza safari ya kuelekea kwenye uzima wa milele, unatakiwa uyajibu maswali haya.

1. JE, MWANADAMU NI NINI? Mwa. 1:26-28, Mwa. 2:7-9

Binadamu ni kiumbe aliye mfano wa Mungu, aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, aliyeumbwa kutokana na mavumbi akatiwa tu pumzi ya uzima ndani yake. Binadamu ni roho, kwa mazingira yoyote aliyopo, ama akiwa hai ama akiwa amekufa. Eze. 18:4 na 20.N NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

2. JE, BINADAMU ANA KAZI GANI? Mhu. 12:13.

Mwanamu anaoutashi wa kuchagua kile anachokipenda, kati ya uzima au mauti. Yuko huru kufanya maamuzi ya kuchagua kwa kuwa Mungu alimpa fursa ya kufanya hivyo tangu mwanzo….Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya, ambao pia ulimaanisha mauti. Ikiwa mwanadamu akimchagua Mungu, basi anapaswa kuitii kila amri ya Mungu na kujitahidi kufikilia ukamilifu wake. Luka. 16:13; Kum. 11:27-28; Mwa. 2:15-17; Mat. 5:48; 2 Kor. 13:11; Yakobo 3:2; Yos. 22:5; Yos. 24:14-15; 1 Nya. 28:9; Yer. 7:23. NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

3. JE, KWA NINI BINADAMU ALIWEKWA HAPA DUNIANI? Kum. 30:19 NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

Imeishajibiwa hapo juu.

4. JE, KIFO NI KITU GANI? Mhu. 9:5; Mwa. 3:19

Kifo ni tendo la kusimama au kunyamaa kwa uwezo wa matendo yote ya shughuli za Binadamu, anapokufa, anakuwa hana tena ufahamu wa namna yoyote ule, anakuwa mfu asiyeishi tena. Anakuwa hajui ni kwa muda gani yumo humo kaburini. Ayubu 3:17; Ayubu 14:12; Zaburi 6:5; Mhu. 12:7; Isa. 38:18; 1 Pet. 1:24; Mithali 11:7; Zaburi 146:3-4; Ayubu 14:21 NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

5. JE, NI KWA NINI TUNAPASWA SISI SOTE TUFE? I Kor. 15:21-22; Ebr. 9-27; Rum 5:12-21.

Watu wote lazima tutakufa kwa sababu tumerithi mauti kutoka kwa Adamu. Wakati Adamu alipomuasi Mungu kwa kula Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya, adhabu aliyopewa ilikuwa ni kifo. Adamu alifanyika kuwa chukizo baada ya kufanya kwake dhambi. Itawezekanaje basi kitu cho chote kibaya kizae chema? Warumi 6:23. NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

6. JE, NI KWA NINI ILIMPASA KRISTO KUFA? Ebr. 9:22; 1 Kor. 15:21-22

Kifo hiki kingekuwa cha milele kama Mungu asingetupatia fursa nyingine. Alimtuma mwanae wa pekee (kwa upande wa Mungu aliyefanywa kuwa mkamilifu, kwa upande wa mwanadamu akifanyika mwenye kuweza kufa) ili kutuwezesha sisi kuwa wana katika jamii yake). Ililazimu awepo mtu wa kutulipia gharama ya kifo cha Kristo, ambaye hakutenda dhambi, alijitolea kulipia gharama kwa ajili yetu kama tukimruhusu. Wakati wote hapa chini kwa zama za miaka yote watu walikuwa wanatoa sadaka za kuteketezwa ili kuonyesha kwamba walimkubali Kristo ajaye hapo siku za mbele yao.

I Kor. 15:12-18; Yoh. 3:16; Yoh. 14:7-11; Rum. 8: 15-17; Gal. 4:5-6; 2 Kor. 5:18-21; Rum. 3:25; Ebr. 4:15-16; Ebr. 5; Ebr. 9:11-14; Yoh 17; Law. 17:14. NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

7. JE, MAUTI YA PILI NI NINI NA INAFANANISHWA NA NINI? Ufu. 21:8; Zab. 37:20

Mauti ya pili ni hukumu kwa waovu ambayo kwayo wataangamizwa ama kuteketezwa kabisa milele .

Ufu. 2:10-11; Ufu. 20:5-6; Ufu. 20:12-15; Yuda 7; Mat. 25:41 & 46; 2The. 1:8-9; Mal.4:1; Ayubu 4:8-9; Ayubu 20:5-8 na 26; Ayubu 21:30; Mat. 13:30 & 40-42; Mat. 18:8-9; Mk 9:43-46; Mit. 2:22; Mit. 10:25-30; Zaburi 37:9-11; Oba. 15 & 16. NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

8. JE, NI NANI ATALAZIMIKA KUFA KWENYE HII MAUTI YA PILI? Ufu. 20:12-15

Wanaolazimika kufa ni wale walioamua kuchagua mauti, kuliko kumtumikia Mungu.

Yoh 15:6; Zaburi 9:17; Zaburi 145:20; Eze. 18:26-28; 2 The. 1:7-9; Hesabu 15:31; Ayubu 8:20 na 22; Ayubu 18:5-17; Zaburi 92:7; Mat. 3: 10; Mat. 7:19. NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

9. JE, ITAKUWA WAPI? 2 Petro 3:7-10

Dunia na waovu wote vitaunguzwa lakini ulimwengu uliobakia utafanywa kuwa Bustani ya Edeni mpya (dunia).

Kum. 32:22; Lk. 12:49; Zaburi 104:35; Isa. 11:4; Isa. 13:9 & 11; Isa. 28:22; Mal. 4:3; Isa. 51:3; Ufu. 21:1; NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

10. JE, WATAKATIFU WATAKUWA WAPI KATIKA MAISHA YAO YA UMILELE? Zab. 37:11

Wapole au wacha Mungu watairidhi nchi milele. Baada ya Mungu kuifanya nchi mpya (kwa kuitengeneza upya ile iliyokuwepo zamani). Mji Mtakatifu Yerusalemu Mpya utashuka kutoka kwa Mungu ukitokea Mbinguni na utawekwa hapa duniani na Mungu atafanya maskani yake pamoja na mwanadamu hapa duniani.

Ufu. 21:1-3; Zaburi 37:9;Zaburi 37:11; Zaburi 37:22; Mathayo 5:5 NI MPYA! (KWENYE MAHUBIRI MAFUPI)

 

RUDI KWENYE KURASA KUU