Je Mwanadamu ni kitu gani?

Je, Mwanadamu ni kitu gani na ni kwa nini viumbe wote waliumbwa hapa duniani, je, yeye anaouwezo wa kuwaza na kufikiri ama kupima mambo? Je, ni kwa nini yeye anaonekana kuwa yu mkuu wa kila aina ya mfumo wa maisha?

Hili ndilo jibu lake. Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake na akampa mamlaka juu ya kila kiumbe kilicho hai kitambaacho juu ya nchi. Kwa hiyo, Mwanadamu anaonekana kuwa bora na atawale juu ya kila kilicho hai kwa kuwa Mungu aliamuru iwe hivyo.

Je, Mwanadamu aliumbwaje na anatokana na nini?

Hapa kuna maelezo makamilifu kuhusiana na uumbwaji wa mwanadamu. Mavumbi ya nchi na Pumzi ya uhai. Hakuna kitu kingine kilichitiwa ndani ya mwanadamu. Mchanganiko huu wa Mavumbi na Pumzi ya uhai ilifanyika nafsi hai. Wakati mwanadamu anapokufa pumzi yake hutoweka na mavumbi yaliyobakia hufanyika nafsi iliyo kufa.

Kwa hiyo tunaona kwamba roho yaweza kufa na kubakia mavumbi tu iwapo ikifa ama yaweza kubakia kuwa mavumbi na pumzi kama ikiwa hai.

RUDI KWENYE KURASA KUU