UKWELI WA KIBIBLIA

Imeandikwa na Herschel Lyda na John Fyfe

 

  1. Fundisho kuhusu Umoja wa Mungu. Kuna Mungu Mmoja tu, ambaye ni Muumbaji wa vitu vyote vilivyoko na ni Baba wa wote wenye mwili. Isaya 44: 6-8; Waefeso 4:6; Wakorintho 8:6
  2. Yesu ni Mwana wa pekee wa Mungu ambaye alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, alizikwa na kufufuka tena kutoka kwa wafu. Yohana 20:31; Matendo 8:37; 1 Yohana 5:
  3. Roho Mtakatifu ni uweza au nguvu za Mungu zitendazo kazi miongoni mwa waumini wa Yesu Kristo. Matendo 1:8; Warumi 8:9,
  4. Biblia ni Neno la Mungu lenye uvuvio ambalo ndilo ndilo njia pekee inayoweza kuwaongoza Wakristo na kuwaonyesha jinsi iwafaayo ukishi. Matendo 3:21; 2Timotheo 3:16-17
  5. Mwanadamu ni kiumbe mwenye kupapatwa na madhila ya maradhi na hatimaye kufa. Na ni kwa kupitia kwa Yesu Kristo tu anaweza kupokea kipawa cha kutodhurika na kufa jambo litakalotokea hapo atakapokuja tena hapa ulimwenguni. 1 Yohana 5:12; Warumi 5:12; Warumi 6:23; Zaburi 146:4; Mhubiri 9:5
  6. Upendo wa Mungu na neema yake vinampatia mwanadamu Wokovu ambao anaupata kupitia kwa Yesu Kristo pamoja na msamaha wote wa dhambi iwapo kama atailinda imani hadi pale atakaporudi tena Yesu Kristo hapa duniani. Yohana 3:16; Luka 9:62; Wafilipi 3:20-21
  7. Mwanadamu anapaswa kumrudia Mungu kupitia kwa Yesu Kristo na kuiamini Injili, kizikiri dhambi, kutubu dhambi zote, kubatizwa kwenye maji mengi kwa jila la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Akiendelea kukua kwenye maisha ya Kikristo na kuvumia hadi mwisho ni jambo la maana. Mathayo 28:19; Warumi 6:4-6; Matendo 2:38
  8. Yesu Kristo anakuja tena na atawafufua wafu, na kuwakirimia kipawa cha kuishi maisha yasiyo na madhila wala kufa wale wote watakao endelea kumtumiki hata mwishao. Pia taanzisha Ufalme wa Mungu hapa duniani. 1 Wathesalonike 4:13-18; 1 Wakorintho 15:51-57; Ufunuo 11:15; Ufunuo 5:10
  9. Kutakuwa na kuangamizwa kwa mwisho kwa wenye dhambi wote. Ufunuo 21:8; Malaki 4:2-3
  10. Kutakuwa na marejesho mapya ya ulimwengu huu na kuwa ni mahali bora pa kuishi kwa kiwango sawa na vile ilivyokuwa imeubwa hapo mwanzoni na kuuweka Mji wake Mtakatifu hapa duniani yaani Yerusalemu Mpya. Matendo 3:21; Ufunuo 21:2-3

REJEA KWENYE UKURASA MKUU