James Herschel Lyda

Je, Baada ya Kifo Nini Kinafuatia?

 1. Wahubiri wanatuambia kwamba mpendwa wetu aliyefariki SASA amekwenda Mbinguni.
 2. Lakini hebu tazama jinsi Biblia inavyosema kwenye Maandiko Matakatifu yafuatayo. Yohana 3:13 Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.

  Zaburi 115:16 Mbingu ni mbingu za BWANA, Bali nchi amewapa wanadamu.

  Zaburi 146:4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hizo mawazo yake hupotea,

 3. Wahubiri wanatuambia kwamba mpendwa wetu aliyefariki sasa anajua kila kitu na anaufahamu mkubwa kuliko alivyowahi kuwa nao huko nyuma.
 4. Lakini hebu tazama jinsi Biblia inavyosema kwenye Maandiko Matakatifu yafuatayo. Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajuaya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

  Zaburi 146:4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hizo mawazo yake hupotea,

  Mhubiri 9:10 Lo lote mkno wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

 5. Wahubiri wanatuambia kwamba mpendwa wetu aliyefariki sasa amekwenda kukutana na wapendwa wengine.
 6. Lakini hebu tazama jinsi Biblia inavyosema kwenye Maandiko Matakatifu yafuatayo. 1 Wathesalonike 4:15 Kwa kuwa twaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakao salia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.

  Matendo ya Mitume 2:29 Wanaume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.

  Mhubiri 9:10 Lo lote mkno wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

 7. Wahubiri wanasema kwamba mpendwa wetu aliyefariki sasa anafurahia sana kuwa kwenye Kiti cha Enzi cha Mungu.
 8. Lakini hebu tazama jinsi Biblia inavyosema kwenye Maandiko Matakatifu yafuatayo. Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

  Mwanzo 3:19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

  Zaburi 6:5 Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakaye kushukuru?

 9. Wahubiri wanasema kwamba mpendwa wetu hayuko tena kwenye hili sanduku la jeneza sasa.
 10. Lakini hebu tazama jinsi Biblia inavyosema kwenye Maandiko Matakatifu yafuatayo. Ezekieli 18:4 Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo roho ya mwana ni mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.

  Warumi 3:23 Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

  Warumi 5:12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hiyo mauti iliwafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;

  Wherefore, as by one man sin entered into the world, and death by sin; and so death passed upon all men, for that all have sinned:

  Ayubu 19: 26 Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;

  27 Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia unazimia ndani yangu!

 11. Wahubiri husema kwamba mpendwa wetu aliyefariki hahitaji tena huu mwili wa kidunia.

Lakini hebu tazama jinsi Biblia inavyosema kwenye Maandiko Matakatifu yafuatayo. Yohana 20: 27 Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete mkono wako uutie ubavuni mwa mwangu; wala usiwe asiye amini, bali aaminiye.

Ayubu 19: 26 Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;

27 Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia unazimia ndani yangu!

Wahubiri husema kwamba mpendwa wetu aliyefariki sasa yupo kwenye mahali pazuri zaidi.

Lakini hebu tazama jinsi Biblia inavyosema kwenye Maandiko Matakatifu yafuatayo. 1 Wakorintho 15:55 Kuwapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?

56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.

Zaburi 30:8 Ewe BWANA, nakulilia Wewe, Naam, kwa BWANA naliomba dua.

9 Mnafaida gani katika damu yangu Nishukapo shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yataitangaza kweli yako?

10 Ee BWANA, usikie, unirehemu, BWANA uwe msaidizi wangu.

Bible inasema hivi:

Mwanzo 2:7 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pmzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Ezekieli 18:4 Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo roho ya mwana ni mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.

Mwanzo 3:19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

Ayubu 21:23 Mmoja hufa katika nguvu zake kamili, Mwenye kukaa salama na kustarehe;

24 Vyombo vyake vimejaa maziwa, Na mafuta ya mifupani mwake ni laini.

25 Mwingine hufa katika uchungu wa roho, Asione mema kamwe.

26 Wao hulala mavumbini sawa sawa, Mabuu huwafunika.

Ayubu 34:15 Wenye mwili wote wataangamia pamoja, Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.

Zaburi 22:29 Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake,

Zaburi 103:14 Kwa maana yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.

15 Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo.

16 Maana upepo hupita juu yake, kumbe haliko! Na mahali pake hapaonekani tena.

Zaburi 104:29 Wewe wauficha uso wako, Wao wanafaidika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao.

Mhubiri 3:19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; maana wote ni ubatili.

20 Wote huenda mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.

Danieli 12:2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.

Ayubu 17:16 Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu, Itakapokuwapo raha mavumbini.

Isaya 38:18 Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.

I Wakorintho 15:12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?

13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka;

14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yetu ni bure.

15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa ni mashahidi wa uwongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.

17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yetu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.

18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.

19 Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.

20 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.

Yohana 5:25 Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.

Yohana 11:25 Yesu akawaambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;

I Wathesalonike 4:13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.

14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.

15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.

16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ta Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, itumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

18 Basi farijianeni kwa maneno hayo.