NYAKATI ZA UPAGANI

Na James Herschel Lyda

Kiswahili III

Profesa Peake Dana

13 Julai 1998

Muhtasari wa Yaliyomo

Maelezo yaliyotafitiwa kisomi: Chanzo au kiini cha ushawishi wa upagani kwenye mila zetu kilianza na kuanzishwa na uhalisia wa kimaisha, na sio kwa namna ya uzushi tu au kwa hulka za kimisisimko kama ilivyozoeleka kudhaniwa kwenye mawazo yz watu.

I. Wana wa Nuhu waliendelea kuzaliwa na kuijaza dunia wakianzia kwenye mji wa kale wa Sumeri.

                 A. Nimrodi, mjukuu wa Nuhu, alijenga himaya kubwa.

   1. Nimrodi aliwakusanya watu pamoja kwenye miji yenye maboma.
   2. Nimrodi aliwawashawishi watu waujenge mnara wa Babeli.
   3. Nimrodi aliugeuza mnara wa Babeli kuwa kitovu cha ibada za kidini.

                B. Dini hii ya watu ilianza kuwa ni kuabudu mizimu. 

   1. Majina ya mungu-Nuhu niyo yalijulikana sana.
   2. Majina ya mungu-Nimrodi yalikuwa mengi nay a namna mbalimbali.

                C.  Nimrodi akaposa mke.

                    1. Jina lake ni Semiramus alikuwa na majina ya miungu yaliyojulikana vizuri sana kama alivyokuwa Nimrodi.

                 D. Kifo cha Nimrodi kiliteta hadithi kubwa.

                    1. Shemu alijaribu kumuua Nimrodi.

                    2. Baada ya kifo cha Nimrodi, mke wake Semiramus alichukua mimba na akazaa mototo.

                 E. Ninus akachukua mahala pa Nimrodi.

                    1. Ninus marries his own mother.

                    2. Semiramus akamuua.

                 F. Dini ya Nimrodi ikaenea hadi huko Misri.

                    1. Osiris ni jina lingine la mungu-Nimrodi lililotumika hukoMisri.

                    2. Seth alimkatakata Osiris vipande.

 

ZAMA ZA UPAGANi

Chanzo au kiini cha ushawishi wa upagani kwenye mila zetu kilianza na kuanzishwa na uhalisia wa kimaisha, na sio kwa namna ya uzushi tu au kwa hulka za kimisisimko kama ilivyozoeleka kudhaniwa kwenye mawazo yz watu.

Ulimwengu mpya ulianzia kwenya milima ya Ararati baada ya gharika kuu iliyotikea kwenye zama za mji wa Sumeri. Nuhu, na watoto wake watatu, Shemu, Hamu, na Yafeti, na wake zao waliondoka alitoka kwenye safina na wakaanza kuzaana na kuijaza nchi. Waliongoka kwenye mlima wa Ararati na wakaenda kwenye nchi tambarare ya Shinari, ambako kulikuwa ni mahala pazuri sana kwa kuishi na panapofaa sana kwa shughuli za kilimo (jarida la Josephus 30). Kadiri watu walivyozidi kuongezeka, ndipo watu walijikusanya pamoja na wakaanzisha koo au jamii na miji.

Miongoni wa wana wa Nuhu, sisi sote tunausikitikia mlolongo wa uzao wa Hamu. Motto wa Hamu alikuwa ni Kushi ambaye alikuwa ni baba wa Nimrodi. "Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA. Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari". (Mwa. 10: 8 - 10). Nimrodi alikuwa ni mtaalamu sana wa kuwinda wanyama na wa kulenga shabaha au pinde (jarida la Ridpath 114 -15). Kwa mujibu wa historia, inasema kwamba kipindi hiki, wanyama waliokuweko juu ya uso wa nchi walikuwa na nguvu sana na wakali kwa wanadamu kiasi cha kuwafanya watu kuhofia sana maisha yao. Nimrodi alifanyika kuwa ni mlinzi wao kwa kazi yake ya kuwawinda hawa wanyama akiwafukuza amepanda farasi akiwa na uta na mishale. Pia aliwakusanya watu wakae kwenye koo na mijini ili awalinde. Alijenga kuta za boma kuzungushia hii miji ili kuwafukuza wanyama na kuwazuia wasiingie (jarida la Woodrow 2 - 4). Kwa ajili hii watu walimuona na kumchukulia Nimrodi kuwa kiongozi wao. Utawala wake ulifika hadi kwenye pwani ya bahari ya upande wa kaskazini mwa Babeli. Mji wake mkuu ulikuwa ni Uru, mwendo kitambo tu na mto Frati. Nimrodi alikuwa ni mtawala wa kwanza wa kizazi cha pili cha Wakaldayo(Ridpath 114 -15).

Flavius Josephus, mwanahistoria wa Kiyahudi alisema kwamba Nimrodi waliwasababisha watu wamuasi Mungu. Nimrodi akaubadili mfumo wa utawala wake na kuwa wa kiimla. Aliwapelekesha kwenye mambo amnayo walimfanya hata Mungu alete gharika na kuigharikisha dunia, kwa kuujenga mnara ufike hadi mbinguni. Ilikuwa uwe mrefu sana kiasi kwamba hata maji ya gharika yasingeweza kufika kileleni kwake. Kwenye mchakato huu wa kujenga mnara, ndipo lugha za watu zikibadilika ili wasiweze kuelewana. Kwa ajili ya kuchafuliwa huku kwa lugha, watu waliacha kuujenga huu mnara. Mahali pale pakaitwa Babeli, maana yake ni machafuko (33).

Baada ya watu kuacha kujenga mnara palipageuza kuwa ni mahali pa kufanyia ibada. Wakaijenga kuba juu ya mnara ambapo palifanyika kuwa ni kitovu cha ibada za kila aina ya miungu lakini sio za Mungu wa kweli, Mimi niko, Mungu Mwenyezi. Hapa kwenye kuba palifanywa kuwa ni mahali pa kujifunzia elimu ya unajimu au utabiri na elimu ya nyota na anga. Palifantika kuwa ni mahala pa kufanyia mambo ya uchawi na matendo mengine yote ya uomu. Palikuwa ni mahali pa kuabudia za sanamu (Wallbank 16).

Dini ya watu wa ufalme huu ilikuwa ni ya kuabudu mizimu. Wazo la dini hii ililitokana na gharika kuu, kwenye safina, na mmoja au zaidi ya watu au roho nane. Watu walijulikana kwa majina ya miungu, kama tunaovyyona mfano mmoja wapo ni kwamba Nuhu alijulikana kama Ziusudra huko Sumeri, na alijulikana kama Utanapishtim na Atra-Hasis huko Akkadi, Abzu katika Sumeri, na pia alijulikana kama Xisouthros huko Ugririki au Uyunani. Mka wa Nuhu alikuwa na jina la mungu aliloitwa la Tiamati. Haya yalikuwa ni majina waliyojulikana kwayo kutoka kwa wazee wao ambao pia walikuwa ni mababu wa Nimrodi. Inaonekana kwamba Nimrodi alijichukulia sifa na majina ya miungu iliyokuwepo huko nyuma na kujiita yeye mwenyewe kwa majina yao. (Graves 56). Nimrodi alikuwa na majina mbalimbali ya miungu zaidi ya hamsini, na jina moja lililojulikana sana lilikuwa ni Marduk (Lambert).

Kwa mujibu wa Enuma Elish, Utendaji wa Uumbaji wa Wababelonia, kulijitokeza mabishano kati ya miungu ya umri mdogo na mkubwa. Tiamat alichoshwa kwa kuwa miungu wenye umri mdogo walikuwa wanapiga kelele nyingi sana, kwa hiyo, aliamua kufanya kitu fulani. Miungu miwili kati yao, yaani Ea na Anu, mtoto wa Nuhu, Hamu na mtoto wa Hamu Kushi, walishindwa kwenye vita dhidi ya Tiamat (Mke wa Nuhu). Kwa kuwa Marduk, ambaye ni Nimrod, alikuwa na sifa kubwa ya kupigana vita kiasi kile, iungu midogo ilimwendea kumuomba aisadie. Nimrodi aliwaambika kwamba angewasaidia kwa masharti tu kama watakubali kumfanya awe mfalme na liongozi wao mwenye nguvu zote za kiutawala na kijeshi ukiwemo uweza wa mambo ya uzima na mauti. Alifanikiwa kwenye mapigano yake dhidi ya Tiamat na aliufanya ulimwengu uwe wa namna aliyoitaka yeye au aliuweka mkononi mwake uwe kama ulivyokuwa kwenye kanuni ya mambo ya uumbaji (Clayton 120). Lakini zaidi ya hayo yote, alifukuzwa aende kwenye kisiwa cha mbali na mume wake Nuhu. Hawa miungu wakamtangaza Marduk kuwa ni mfalme wao, na akayataja majina yake hamsini. Marduk alikuwa akimrejesha kila mwaka kwenye wadhifa wake wa mfalme wa miungu kwa mujibu wa taratibu za maadhimisho ya sherehe za Mwaka Mpya kwenye Nyumba ya Akitu wakati taratibu za uanzishaji zikinuiziwa. Kuongezeka kwa uwiano wa Marduk na miungu mingine muhimu wa hekaluni kumeelezwa kwenye gombo dogo la maandiko asilia ya zamani (aina ya gombo zenge umbo la mchongoko zilizotumiwa kuandikia nyingi zake zilikuwa ni za udongo wa mfinyanzi) ambayo inafafanua kuwa kila mmoja wa miungu hawa alikuwa ni kiungo kinachojitegemea, cha Marduk mwenyewe (Lambert).

Nimrodi alikuwa na ofisa wa jeshi lake aliyekuwa na mke mzuri sana mwenye nywele za rangi ya shaba. Hadithi za kale zinasema kwamba alikuwa ni mwanamke mzuri sana kuliko wote waliokuwepo wakati huo (Hislop 74). Hivyo basi, Nimrodi alimtaka, kwa hiyo alimchukua kutoka kwa mume wake yaani yule kapteni wa jeshi na akamfanya kuwa mke wake. Hii ndio moja ya ndoa za kuchanganya damu kuwahi kutokea katika historia ya ulimwengu. Mtu mweusi alioa mwanamke wa kizungu mwenye nywele za shaba (Hislop 229). Jina lake aliitwa Semiramus na jina lake la uungu aliitwa Ishtar. Walijenga hekalu lenye kuba na kumuabudu yeye humo.

Haijulikani bado kama ni nani kati Nimrodi au mke wake aliyeanza kufundisha watu, lakini watu walifundishwa kwamba Nimrodi alikuwa mungu wa jua aliyeshuka kutoka mbinguni na kuchukua au kuvaa mwili wa kibinadamu hapa duniani (Hislop 229). Nimrodi alishirikishwa kwenye mambo mengi ya kichawi na kishirikina na alikuwa akitajwa jina lake kwenye matambiko na manuizo mbalimbali. Alijulikana pia kwamba alikuwa ni bwana wa mazindiko. Alianzisha shughuli za kupiga pinde na aliwafundisha wanajeshi jinsi ya kulenga shabaha. Kwenye mji wake mkuu aliujenga mnara mrefu ambao watu wete walioishi kwenye nchi tambarare ya Shinari wauone na waujongelee. Aliujenga mnara wa matofali yaliyokaushwa na jua, kwa kuwa hakukuwa na mawe yaliyopatikana kwenye uwanda tambarare wa Shinari, na kuyapaka ndani na nje kwa lami (mafuta mazito), ili yasiingiwe na maji. Biblia inseam kwamba watu walijaribu kuujenga wakinuia wafike mbinguni (Mwa. 11: 4) (hii inamaana ya kufika kwenye kiti cha enzi cha Mungu, au watawale kama miungu). Mnara wa hekalu ulijulikana kwa jina la Entemenanki na ulihusiana na Mnara asilia wa Babeli. Lilijulikana kama hekalu la Marduk. Ndani yake mlikuwa na sanamu kubwa la dhahabu ngumu la Marduk na kitanda cha dhahabu ambamo sherehe za arusi zilikuwa zikifanyika. Ibada hii ilinajisika sana kwa taratibu za kingono zilizokuwa ndio maana yake na ndiyo ilikuwa ni namna pekee ya kuitimiliza, ambako kwamba mwanamke alitakiwa aende mara nyingi nyakati za usiku ili akakutane na kufanya matendo ya kingono na miungu (Frazer 142).

Miongni mwa wana wa Nuhu, Shemu ndiye aliyekuwa akimwabudu Mungu wa pekee na wa kweli, Mimi Niko, ambaye ni Mwenyezi. Shemu alijionyesha wazi kwa maamuzi yake ya kumcha Mungu wa kweli kiuwazi kabisa, na ambaye aliitisha mkutano akiwaita wale wote waliodhamiria kumuabudu Mungu wa kweli. Wakaamua kwamba ni lazima Nimrodi akome na kuacha na ndipo walimkamata, wakamshitaki kwa makosa ya jinai aliyoyafanya na hatimaye wakamuua kwa mkata vipande vingi. Kuna wanaosema na kuamini kwamba vipande vile viliteketezwa kwa moto na wengine wanasema kwamba haikuwa hivyo, lakini kuna ukweli mmoja unaokubaliwa na wote, ambao ni kwamba vipande hivi vilipelekwa kwenye miji yote na vilionyeshwa kwa kila mmoja ili view mfano au onyo kwa wale wote wanaothubutu kukataa kumuabudu Mungu wa kweli (Hislop 63). Ikumbuke habari hii kwa kuwa utaiona imerudiwa kwenye desturi moja ama dini na nyingine kukiwa na tofauti ndogo sana.

Baada ya kifo cha Nimrodi, Semiramus alitamalaki na kuanzisha tena dini ya kipagani ya kuabudu jua. Kitambo tu baada ya kifo cha Nimrodi Semiramus alipata ujauzito. Akadai kwamba mwali wa jua umemwingia na kumpatia ile mamba na kwamba Nimrodi mwenyewe yule yule atazaliwa tena au atarudi tena kwa kupitia njia ya kuzaliwa na yeye (Hislop 305). Akamwita yule mtoto wake Ninus, ambaye hatimaye alikuja kuabudiwa kama mungu Nabu. Na baada ya kufikia mri mkubwa kdogo Semiramus aliamua kuolewa naye kwa madai kwamba hata hivyo, alikuwa ni yule yule mume wake Nimrodi aliyezaliwa upya kwa kupitia tu kwake yeye (Hislop 22).

Ninus alisimuliwa kwamba Shemu ndiye aliyemuua baba yake, kwa hiyo alitafuta namna atakavyojilipiza kisasi cha kumuua. Hatimaye walipokutna, vita kubwa ikaanza. Katika vita hii Ninus alifanikiwa kumtoa korodani Shemu, lakini Shemu alifanikiwa kumtoa jicho Ninus (Hislop 63 - 5). Hii ndio sababu inayopelekea kwamba "Wadjat" au nembo ya jicho la Mungu itumike na wengi ulimwenguni kote, hata kwenye nembo ya hela yetu ya dollar ipo.

Semiramus na Ninus walitawala kwa pamoja kwenye kiti cha enzi cha ufalme wa Babeli kwa kipindi fulani. Katika kipindi hiki Semiramus alichukua cheo cha Nimrod; cha ukuu wa wapiga pinde, mjenzi wa miji yanye maboma, shuja mkuu, nk. (Hislop 31). Semiramus alikuwa myawala katili na muimla ambaye hakuzuiliwa na kitu chochote kutimiliza matakwa yake. Baadaye kidogo, Ninus hakuweza kumtimizia mahitaji yake ya kunyumba Semiramus kwa hiyo alimuua, lakini aliendelea kutawala kwa kipindi cha miaka mingine mingi akiwa anaitwa kwa cheo kama Mama Mkuu

Mungu-mke, Ishtar. Wakti wa kipindi cha kutawala kwake alifahamiana na wanaume wengi sana akiwemo baba mkwe wake. Pia kulikuweko na wanaume wengi sana aliowaua. Simulizi zinasema kwamba Semiramus alikutana na Gilgamesh, mfalme wa Wababelonia aliyeishi kwenye mji wa Uruk, na alimueleza jinsi anavyompenda. Lakini Gilgamesh alimkatalia pamoja na kwamba alimtishia kwamba kama atamkatalia basi atamuua kama alivyowafanya weingine wengi aliowapenda na kumkatalia (Clayton 88-91).

Dini hii ya kale ya kipagani ilishamiri sana huko kwenye nchi ya kale ya Babeli wakati ule Mungu alipowachafulia lugha zao kwenye ujenzi wa mnara wa Babeli, na hatimaye dini hii ilienea ulimwenguni kote. Hapo mbele tutajionea jinsi dini hii hii ilivyoanzisha katika Misri ya kale. Semiramus anatajwa kwamba alionekana mara nyingi huko Misri, moja ya kuonekana kwake alikuwa anamponya mmoja wa wanafamilia wa jamii ya kifalme (Hislop 305). Tukio hili pia lilisaidia kushamiri kwa dini hii katika nchi hii ya Misri.

Wamisri wa zamani waliamini kwamba mungu wa jua aliitwa Aten au Re jina ambalo hatimaye liliunganishwa na kuwa Aten Re. Hatimaye iliaminika kwamba alishuka duniani na kutawala kwenye ufalme akiwa kama mungu Osiris, hili lilikuwa ni fundisho lilelile ambalo Nimrodi aliwafundisha watu wa Babeli. Mungu-mke aliyekuwa anatawala sambamba nay eye aliitwa Isis. Simulizi za kale zinatuambia kwamba ndugu-mume wa Osiris yaani Seth alimuua na kumkatakata vipande vya mwili wake na kuvitupa kwenye mto Nile. Isis alivitafuta vipande hivyo hadi akavipata karibu vyote isipokuwa kimoja tu alikikosa kabisa ambacho ni zakari yake au uume. Na mara tu baada ya kukipata aliitumia hadi ilimpatia ujauzito. Baada ya kumzaa mtoto wa kiume, alimuita Horus (Wallbank 25 - 26).

Horus akasimuliwa hadithi kwamba Seti alikuwa ndiye aliyemuua baba yake na akajifunga kujilipizia kisasi kwake. Alipigana vita vibaya sana ambayo matokeo yake Seth alihanithiwa na jicho la Horus lilinyofolewa (Clayton 103 & 170).

Je, hii haifanani na habari ile tuliyokwishaioma kutoka Babeli? Jambo hili hili lilirudiwa kwa namna mbalimbali kutokana na mapokeo ya sehemu moja hadi nyingine. Baada ya Misri dini hii ilienea na kushamiri huko Ugiriki au Uyunani hadi Rumi. Iliendelea kushamiri kupitia kwenye imani za kipagani za kale hadi ilipofikia kuingizwa kwenye imani ya Kikristo au kwenye Ukristo na hatimaye dhana ya Ukristo ikabadilika kuwa Upagani. Baadhi ya mafundisho yale yale na mapokeo aliyoyaanzisha Nimrodi yanaonekana yakitumiwa kwenye mashirika ya kidini karibu zote hapa duniani hata leo.

 

Waliohusika kutupatia maelezo ya kazi hii ni: (Kama walivyo kwa Kiingereza),

Clayton, Peter. Great Figures of Mythology. New York: Cresent. 1990.

Frazer, Sir James. The Golden Bough. Denmark: Wordsworth. 1993.

Graves, Robert. New Larousse Encyclopedia of Mythology. New York: Promethus. 1959.

Hislop, The Rev. Alexander. The Two Babylons. Neptune: Loiyeaus. 1959.

Josephus, Flavius. Josephus: Complete Works. Standard ed. Trans. William Whinton. Philadelphia: Porter and Coates. 1984.

Lambert, W. G. and A. R. Millard. "Atrahasis." 1969. Reading the Old Testament, the Electronic Edition. Online. Internet. Available http:// hope.edu/academic/religion/bandstra/RTOT/CH1/CH1_2A3C.HTM (8 July 1998).

Ridpath, John Clark. History of the World. Vol 1. Cincinnati: Ridpath Historical Society. 1936. 9 vols.

Wallbank, T. Walter, Alastair M. Taylor, and Nels M. Bailkey. Civilization Past and Present. Chicago: Scott, Foreman, and Co. 1962.

Woodrow, Ralph Edward. Babylon Mystery Religion. Riverside: Woodrow. 1993.

 

Baadhi ya vyanzo vya Nukuu zetu kuhusu Wavuti za Nimrodi (Hawakubaliani kwenye "Ukweli")

 

RUDI KWENYE KURASA KUU