NGOJEA TU

 

Nasimama kwenye njia panda,

Wakati jua likizama jioni taratibu,

Nikingojea ishara ya taa ziongozazo iniruhusu,

Na alama ya tahadhari iondoke.

 

Ingawa nalazimika kuivuka Yordani,

Hakuna mtu wa kuchukua mahala pangu,

Neno hili aliambiwa Adamu,

Na wanadamu wengine wote waliofuatia.

 

Na kisha kitakuja kipindi cha kusinzia na kulala,

Lakini kitakuwa ni kama njozi tu,

Tulalapo katika Yesu,

Tutakapokuwa tumeishavuka mto wa giza wa Yordani.

 

Lakini naona dalili ya asubuhi yenye baraka,

Ikipenya kwenye usiku huu wenye huzuni,

Na ufufuo mtukufu,

Wakati Kristo atakapozivunja nguvu za mauti kuzimuni.

 

Pale nitakapo ishikilia taa yangu sawia na ikiwaka,

Na ikiwa na mafuta yake tele,

Sitafanana na wale wanawali wapumbavu,

Nikafungiwa nje ya mlango nisiingie.

 

Nakungojea kurudi kwake Kristo,

Na parapanda ya Mungu ikilia,

Kuakapokuwa na sauti na nyimbo za furaha,

Ambapo wateule wake wote watakusanyika pamoja,

 

Na: Hilliard C. Case

Rt 1, Flat Rock, NC

REJEA KWENYE UKURASA MKUU