Utoaji wa Zaka na Sadaka

Na James Herschel Lyda

Zaka maana yake: ni tendo la kutoa asilimia kumi au moja ya kumi ya mapato yako na kuitoa kanisani.

Sadaka maana yake ni: tendo la kujitoa; ni mchango muhimu unaotegemewa kwa ajili ya kulitegemeza kanisa na iko mbali na zaka, inatakiwa itolewe kwa moyo wa hiyari na shukurani. Zaka na sadaka ni za muhimu kwa ajili ya kulitegemeza kanisa liweze kuwa na maendeleo na kutegemeza watumishi wa Mungu wanaolihudumia kanisa.

Waebrania 7:1 Kwa maana Melikizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;

2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, na tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;

3 hna baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.

4 Basi angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yenu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara.

5 Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo na sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu.

Tendo hili la kumtolea Mungu zaka, au kuwapa watumishi wake lilikuwa linafanyika kwa wachamungu wa zamani hata walioishi zama zilizokuwa kabla ya sheria na amri za nabii Musa. Baba yetu Ibrahimu alizitoa kwa Melkizedeki zaka za mali alizoziteka vitani, na Yakobo aliweka nadhiri kwamba hataacha kumtolea Mungu zaka zote za kila kitu ambacho Mungu atambarikia.

Mwanzo 28:20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu. 22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

Katika kipindi kile cha Sheria, zaka zote zilitolewa kwa Walawi; ndio waliozikusanya na kuzitunza au kutumia zaka zote zilizotokana na mazao au mapato yao. Kila mnyama wa kumi katika wale waliopita chini ya fito ya fimbo alitolewa zaka.

Walawi 27:30 Tena zaka zote za nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA.

32 Tena zaka yote ya ng’ombe, au kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa BWANA.

34 Haya ndiyo maagizo, BWANA aliyomwangiza Musa kwa ajili ya wana wa Israeli katika mlima wa Sinai.

Hesabu 18:21 Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithiwao, badala ya huo utimishi wautumikao, maana, nihuo utumishi wa hema ya kukutania.

23 Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi.

24 Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.

25 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwa zaka mkononi mwa wana wa Israeli, niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wwenu, ndipo mtakaposongezayo sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.

Mwishoni mwa ‘mwaka wa utoaji,’ kila aliyemtolea alitoa tamko takatifu akitangaza mbele za Mungu akisema kwamba amejitahidi kukamilisha amri na sheria alizoziamuru Mungu na kamwe hakuacha kumtolea kwa kuficha nyumbani kwake ili atumie mwenyewe kiasi chochote cha sehemu ta zaka iliyostahili aitoe kwa Mungu. Na kwa ajili hiyo, alistahili kumfanyia Mungu maombi maalumu akimuomba ambariki kutoka mbinguni, makaoni mwake na awabariki watu wake Israeli. Moja ya shutuma mbazo Israeli walikabiliana nazo katika siku za mwishoni mwa Agano la Kale ilikuwa ni kwamba walimuibia Mungu, kwa kuwa hawakumtolea zaka na dhabihu; na kwa hiyo taifa lao lote lilikuwa "limelaaniwa kwa laana." Lakini kama wangalizileta zaka kwenye nyumba ya Mungu, na kumjaribu kwa njia hiyo, wangebarikiwa vitu vingi kiasi kwamba wangekosa hata mahali pa

Malaki 3:7 7Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gain?

8 Je! Mwanadamu atamuibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gain? Mmeniibia zaka na dhabihu.

9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukusha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.

12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana watakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi

Hivi leo tunashangaa tunapoona mazao yetu yanashindwa kutoa mazao mengi na mvua inaposhindwa kunyesha na inaponyesha huja nyingi zaidi ya inavyohitajika kiasi cha kufanyika sababu ya kuharibu na kuangamiza mazao na maisha pia. Inaonekana kwamba hatuwezi kujiepusha na uharibifu wa hali ya hewa na maafa mengine zinazotufika kwa karibuni kila siku. Jibu lake liko kwenye aya nilizozitaja hapo juu. Mmemwibia Mungu kwa kutotoa zaka na dhabihu zake. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Hivyo basi, ni wajibu wetu tulioamriwa kuyasaidia makanisa yetu, wachungaji wetu, na kazi zao wanazomtumikia Mungu kwa njia ya zaka na sadaka zetu. Tukidhani kwamba sisi hatuna kiasi cha kutosha kutoa zaka, hiyo inasababishwa na hali yetu ya kutomtolea Mungu zaka zetu kikamilifu. Kumbuka amesama kwamba tukimtolea zaka kamili, yeye atatubariki kiasi kwamba totakosa mahali pa kuziweka kwa vile zitakavyofurika kwa wingi. Hizi zaka tunazozitoa zinatakiwa zitumike kwa kusaidia maendeleo ya kanisa la mahali pamoja na na watumishi wake na pia zinatakiwa kutumika kusaidia mtandao wote wa makanisa na watumishi wa Mungu. Kristo aliwamuru wanafunzi wake wasichukue dhahabu yoyoye, wala fedha mishipini mwao kwa kuwa mahitaji yao yote watapewa.

Mathayo 10:9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mshipini mwenu; 10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake.

Mtendakazi amtumikiaye Mungu anastahili apewe ujira wake. Ikiwa yeye ni mtumishi wa kweli wa Mungu, anatakiwa asaidiwe na kwa njia ya zaka zetu. Ni mri iliyotolewa na Mungu mwenyewe kwamba tunapaswa tutoe zaka na kutoa sadaka ili kuisaidia Nyumba ya Mungu na watenda kazi wake.

REJEA KWENYE UKURASA MKUU