Amkeni Enyi Wamarekani!

Na: Herschel Lyda

1 Februari, 2006

Pamoja na maafa yote yanayoikumba na kuiathiri nchi hii ka kipindi kitambo kilichopita, je, sio jambo la busara kwetu kujiuliza NI KWA NINI? Upande mmoja wa taifa letu unakumbwa majanga ya ukame na muunguo wa moto wakti ambapo pande nyingine za nchi kukiwa kunanyesha mvua kubwa kiasi cha kusababisha mafuriko na kusababisha maporomoko ya udongo. Kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita tumejionea majanga kadhaa ya tufani kubwa kubwa, vimbunga, mafuriko, matetemeko ya ardhi, kupoteza kwa mazao ya kilimo, matendo na matishio kadhaa ya kigaidi kwa kiasi ambacho nchi hii haijawahi kupitia kamwe huk nyuma. Mtu anaweza kujiuliza kwamba je, Mungu ametugeuzia kisogo na kutuacha? Na kwamba je, hivi amekataa kabisa kutulinda na majanga haya yote mabaya yanayotokana na uasili maumbile ya dunia hii?

Kuanzia pale uanzishwaji wa nchi hii kuwa taifa lenye kauli mbiu ya "Mungu Ndiye Tumaini Letu," tumekuwa tukibarikiwa sana kwa namna mbali mbali. Tumekuwa ni taifa lenye nguvu nyingi sana kwenye uso wa hii dunia. Kwa kupitia uwezo hali hii ya uwezo mkuu, tumeweza kuubadilisha ulimwengu wote kwa namna moja ama kwa ile nyingine. Tumekuwa ni kiini cha mambo ya kilimo hapa duniani. Tulitoa chakula cha kutosha kulisha karibu mataifa yote. Kuna kipindi ambacho tulikuwa ni kiini cha shughuli za ufumaji na utengenezaji wa nguo duniani. Tulitengeneza nguo na kuvalisha karibu watu wote duniani. Tulitengeneza karibu mashine zote zinazotoa nguvu kuleta maendeleo ya dunia, kwa wakati mmoja. Mataifa mengine mengi hapa duniani yanawadharau Wamarekani. Lakini tumefikia ukomo wetu na sasa badala yake tunashuka chini. JE, NI KWA NINI?

Ilianza kwa kupata mwanya kidogokidogo kwenye jamii zetu kwanza kwa kufundisha kwenye shule zetu mawazo fikirika ya elimu ya mageuzi ya kimaubile, yaliyoanzishwa na Darwin mnamo mwaka 1859. Elimu hii ilionyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye vitabu vya kujifunzia mnamo miaka ya kwanza kwanza ya 1960. Elimu hii ilianzia kwa kudharau imani ya Biblia na uwepo wa Mungu. Halafu kukafuatiwa na tafsiri ya liberali ama tafsiri huru ya marekebisho ya kwanza ya kuachilia mambo yote na mienendo yote isiyo ya kimungu kufanyika.

 

Muswada wa Haki wa Katiba ya Marekani

Sahihisho I

Bunge la Kongresi halitaweka sheria yoyote yenye nia ya kuheshimu uanzishwaji wa dini, au kukataza uhuru wa namna yoyote ile; au kuzuia uhuru wa kuongea, au wa vyombo vya habari; au haki ya watu kukusanyika pamoja kwa amani, na kuilalamikia serikali isikilize ili irekebishe malalamiko na kero zao.

Je, ni kwa nini maneno hayo yalitiwa kivuli hapo juu yasitafsiriwe kwa kumaanisha kwamba "Sheria inaweza kutafsiriwa au kuanzishwa kwa lengo la kuzuia uhuru wa kujieleza kuhusu Mungu au amri na sheria zake?" Imetafsiriwa kwa kumaanisha kitu tofauti kabisa na vile inavyosema. Hebu tazama hapo chini isemavyo:

Kilichofuatia baadaye ni kuondoshwa maandishi ya Amri Kumi za Mungu toka kwenye majengo yote ya umma na kupigwa marufuku kufanyika kwa maombi au sala ya wazi karibu kwenye maeneo yote yanayomilikiwa na umma; hasa kukiwemo mashuleni. Kwa matendo haya yote tumeweza kumuondoa Mungu kutoka kwenye maisha yetu na kuwafundisha watoto wetu kumkataa Mungu na mafundisho yake au angalau kwa kuyadharau.

Iwapo kama hatugeuka na kutarejea kwenye njia zetu kwa kumgeukia na kumuabudu Mungu wa pekee na wa kweli na kuzishika amri na sheria zake, basi tutazidi kudhoofika kama taifa. Tutakuwa ni wadogo katika nguvu za dunia na magonjwa yote na majanga ya mataifa madogo yatatuandama. Dalili za kutokea kwa haya zimeishaanza kutokea tayari hapa Marekani. Sehemu kubwa ya dunia haituheshimu au haituoni sisi kuwa ni sehemu ya kujipatia ahueni au ya kupatia msaada tena. Bali sasa wanatulaani na kujaribu kuiangamiza hii Marekani. Inaonyesha kwamba tumeshinda vita yetu ya mwisho. Hatutaweza tena kuishinda hata nchi ndogo sana, kama vile Viet Nam au Iraq.

Hebu basi sisi site tukiwa kama taifa, na kabla hatujachelewa, tuirudishe kwa vitendo ile kauli-mbiu yetu ya "Mungu Ndiye Tumaini Letu." Hebu basi kwa mara nyingine tena tuyarudishe mafundisho kutoka kenye Biblia yawe kama kitabu cha kutumia mashuleni mwetu, kama ilivyokuwa kwenye siku za mwanzo wa kuanzishwa kwa taifa letu. Hebu na tuanzishe tena utaratibu wa kuweka nakala za Amri Kumi za Mungu na machapisho mengine ya maandiko matakatifu na kufundisha kwenye shule zetu, zikiwa kama ni urithi wetu tunaojivunia kwa kauli mbiu yetu ya "Taifa Moja Chini Ya Mungu."

Kumbukumbu la Torati 11:18 Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu.

Watu! Huu ni wakati muhimu sana kwetu wa kudai kuangaliwa upya kwa Mahama yetu Kuu ili iamue suala la kuabudiwa kwa Mungu wa Pekee na wa Kweli.

 

REJEA KWENYE UKURASA MKUU