Je, Uhuru Maana yake nini?

Sikuweza kufanya uamuzi wa kuzaliwa au kujichagulia aina ya daraja la maisha nitakalokuwa nalo maishani mwangu. Lakini Mungu alitupa sisi sote, uhuru wa kuamua kuishi (maisha) au kuwa vinginevyo (yaani kufa). Kumbukumbu la Torati 30:19, inasema: Nazishuhudia na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako:

Ni uchaguzi ulio huru ambao hauna shuruti wala usio na mabembelezano. Huu ndio uhuru kamilifu, unaoendana na kupewa fursa ya kujichagulia hatima ya maisha yako bila ya kulazimishwa.

Sikuwa na fursa ya kujiamulia kuzaliwa kwenye moja wapo wa Jimbo lolote la Amerika au katika nchi nyingine iwayo yote. Mungu na wazazi wangu ndio waliosaidia mimi kuwa hivyo. Sasa nina uhuru wa kuamua nikiwa katika dunia hii ya kupendeza, iwapo kama napenda kufa au kuishi. Bado nachagua Majimbo haya ya Amerika kwa kuwa ni sehemu pekee miongoni mwa mataifa ya dunia hii ninapoweza kupewa fursa ya kipekee ya kujiamria mambo. Ni uamuzi wangu kuchagua aina ya uhuru wa kuishi kati ya kufuata haki au ubaya. Mathayo 6:24 inasema: Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Huwezi kumtumikia Munguna mali.

Sisi tukiwa kama taifa tuna uhuru wa namna ile ile. Tuko huru kuishi kwa kufuata mujibu wa maagizo yaliyoko kwenye amri za Mungu na sheria zake, au uhuru wa kuishi maisha yaliyo nje na kanuni zake za maisha ama hata kumkataa yeye Mungu. Iwapo sisi kama taifa tukimkubali yeye, tunapaswa pia tuzikubali amri na sheria zake na kuzishika. Iwapo kama tukizishika, basi tutabarikiwa zaidi ya hali zetu za ufahamu wa kawaida. Lakini sisi tukiwa kama taifa tunaodai kuwa tunamtii na kumkubali Mungu lakini huku tukiwa hatuzishiki sheria na amri zake, tutapatilizwa na aina zote za magonjwa ya Wamisri.

Kutoka 15:22 inasema: Musa akawaongoza Israeli na mbele kutoka Bahari ya Shamu; nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.

23 Walipofika mahali alipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina likaitwa Mara.

24 Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?

25 Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonya huko; 26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio wasikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimisitatia juu yako maradhi yo yote niwatiayo Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.

Kumbukumbu la Torati 7:12 inasema: Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;

13 naye atakupenda na kukubarikia na kukuongeza; tena atakubarikia uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, maongeo ya ng’ombe zako, na wadogo wa kondoo zako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa.

14 Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo.

15 Na BWANA ayakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao.

Kumbukumbu la Torati 28:15 inasema: Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizayo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.

21 BWANA atakuambatanisha na tauni, hata atakapokweisha kukuondoa katika nchi uingiayo na kuimiliki.

22 BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie

27 BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupona.

Kumbukumbu la Torati 28:59 inasema: ndipo atakapofanya BWANA mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.

60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.

61 Tena lika ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo BWANA juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa.

Mambo ya Walawi 26:21 inasema: Nanyi ikiwa mwaenenda kingume changu, wala hamtaki kunisikiza; nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, kama dhambi zenu zilivyo.

 

UKIMWI – Kwa sasa inakubalika kwamba ugonjwa wa UKIMWI umetokana na Wasimiani (kima) virusi vinavyopunguza nguvu za mwili kujikinga na naradhi (VVU). Kwa mfano, VVU-2 vinahusiana na virusi ambukizi vinavyozuia nguvu za mwili kujikinga na maradhi vya kisiami vinavyogunduliwa katika kima aina ya vipele vya kimangabe (SIV sm), ambao wakati mwingine hujulikana kama kima wa kijani, ambao asili yao ni Afrika magharibi. Fungulia tovuti ya http://www.avert.org/origins.htm

AINA ZA MARADHI YA NDUI: NDUI YA WANADAMU; YA KIMA; YA KUKU; NK. – Magonjwa haya yote huoneana kwa athira ya ngozi. Magonjwa haya husababishwa na virusi vya ndui, hususani ndui kali inayosababishwa na mbung’o hawa wamekuwa wakiogopwa kwa muda mrefu sana wakiaminika kuwa ni mawakala wanaobeba maradhi hatari. Hata kipindi kile cha himaya ya Wamisri, inaaminika kuwa ugonjwa huu wa ndui ndio uliomwua mfalme wa Misri aitwae Farao Ramses V mnamo mwaka 1157 K.K. Ugonjwa huu wa Ndui ya Binadam na Kima au Human Monkeypox

Mfano wa maradhi haya ya ndui hii ya binadamu na kima iligunduliwa katika ukanda wa Afrika Magharibi na Kati katika mwanzoni mwa miaka ya 1970's. Maradhi ya ndui yalikuwa yameisha tokomezwa tayari na kuondolewa kwenye ukanda huu, lakini ishara na dalili zake zilifanana sana. Maradhi haya ya ndui ya kima yameaminika na kuchukuliwa kama zoonosis adimu, na ingawa chanjo inaweza kuzuia kuenea kwa kwa maradhi haya, ni marachache sana imeaminika kwamba yanaweza kukoma pasipo chanjo na hivyo haifai kudharau umuhimu wa chanjo. Waweza kufungua tovuti hii kwa maelezo zaidi: http://www.stanford.edu/group/virus/1999/reynafue/history.html

A. Kundi hili la panzi hukaa kwenye nchi kavu za Afrika Kaskazini.

B. Kwa kipindi, ongezeko huunda na kufikiliza viwango vikubwa na kila kundi huchukua nafasi yake kipekee.

Hii inaitwa mkondo mkuu na mpana na nzige wanajitafutia chakula cha akiba. Kwa mujibu wa Kitabu cha Rekodi za Wadudu cha Chuo Kikuu cha Florida. (http://ufbir.ifas.ufl.edu),

nzige wa jangwani hushikilia rekodi za aina zote mbili yaani kuingia kwa makundi haya makubwa na warefu sana.

1. Mnamo siku za mapema ya mwaka wa 1954, makundi yaliyoishambulia Kenya yalilifunika eneo la kilometa 200.

Hatima iliyo kadiriwa ilikuwa ni kiasi cha takriban idadi ya milioni 50 kwa kilometa ya mraba, wakifanya idadi yao iwe ni jumla ya hesabu ya bilioni 10 kwa kundi lile.

2. Makundi haya yalifanywa kuwa ni vikundi vilivyoambatana kwa siku kwadhaa au kwa majuma kwa zaidi ya kiasi cha maelfu ya maili.

Hadi kufikia mwezi wa Octoba 1988, walipatikana kwa idadi kubwa walifika kwenye maeneo yaliyo karibu na pande za kaskazini kutoka kwenye visiwa vya Mt. Croix huko West Indies, na pande za kusini mwa pwani ya nchi zilizoko katika Amerika ya Kusini za Surinam na Guyana. Kasha waliwasili mmoja mmoja waliletwa na mawimbi ya kitropikali yaliyovuma taratibu ambayo hatimaye yalitotoa viluilui na kuenea kwa nguvu. Umbali walioutumia katika kusafiri kutoka kwenye pwani ya magharibi mwa Afrika hadi kufikia kwenye visiwa vya West Indies ulikuwa ni takriban kilometa 4500.

3. Makundi haya ya Naige wa Jangwani yamenukuliwa kuwa yanaonekana kila mwaka tangu mwaka wa 1860. Kipindi refu kuliko vyote kushuhudia maafa kiliishia mnamo miaka ya 1950-1962.

Nukuu za muonekano wa nzige katika Amerika kwa karne ya kumi na tisa.

1. Wafanyakazi wa huduma za kujitolea walioweka makazi yao kwenye Uwanda Mkuu walikuwa jamaa wagumu sana, wakiathiriwa na ukaufu wa majira ya joto na adha za majira ya baridi. Lakini maradhi yaliyoletwa na panzi kwenye miaka ya 1870 yalikuwa nje ya uwezo wao wa kuyakabili. Hii ni kwa mujibu wa jarida la Melanoplus spretus, pazi wajulikanao kama wa Miamba ya Milimani. Walipita ndani kwa ndani kuoka Dakotas hadi pande za kaskazini ya Texas.

2. Haya yalikuwa ni makundi mabaya sana kiasi kwamba yaliweza kusimamisha gari moshi. Wafanyakazi wa huduma za njia za reli walilazimika kuyaondoa masalia yao toka reli zilizopata joto ambazo kwazo walipendezwa nazo, kwakuwa walisababisha magurudumu ta garimoshi yateleze na kuathiri uwezo wake wa kuvuta garimoshi. Kuliripotiwa jambo hilo hilo kuwa lilitokea huko Afrika Kusini katika miaka ya 1960. Kwa maelezo zaidi soma kwenye tovuti hii: http://64.233.161.104/search?q=cache:onLgDM6aqrYJ:entomology.wisc.edu/bugnet/Lecture%252031%25202003%2520grasshoppers.pdf+%22history+of+locusts+%22&hl=en

Hadi kufikia ujio wa mwanzo wa maradhi ya UKIMWI, ukoma ulikuwa ni ugonjwa mbaya sana wenye kuambukiza. Hata leo, bado unashambulia maisha ya mamilioni ya watu, wengi wao waliwa ni wale walioko Amerika ya Kusini, Afrika, na katika nchi za Pande ya Mashariki. Maafa Mabaya Meusi yaliyozikumba nchi za Ulaya kwenye miaka ya karne ya 14, yakiua theluthi moja ya watu, yalikuwa ni chukizo kuu sana ya kuweza kukumbukwa. Lakini yalikuja na kuondoka haraka, kama vile tetemeko kuu la ardhi, lililofuatiwa na mlolongo wa mambo baada ya mshituko. Soma tovuti ya: http://pandoras-box.org/my05002.htm Nchi ya Amerika inaaminiwa kuwa ni ya tatu duniani kwa kugundulika visa vya maambukizo ya wakoma. Soma tovuti hii: http://www.who.int/lep/stat2002/global02_files/lep04.xls

Kuna idadi ndogo tu ya maradhi yanayokuja yakitokea barani Afrika (Misri) lakini tunapoyaona maradhi haya yakiwa kwenye nchi yetu, basi ni ishara tosha kuonyesha kwamba tumekwisha mkubali Mungu wa pekee na wa kweli ndiyo, lakini hatuzishiki amri na sheria zake. Ama kwamba, hatujaachana bado na ile hali ya kuiandama miungu mingine au ni kwamba hatuja kidhi kiwango kinachohitajika katika kukusanyika pamoja na kumuabudu yeye Mungu wa pekee wa kweli na kuzishika kikamilifu amri na sheria zake. Kama tungekuwa sisi ni taifa la kipagani basi angegeuza use wake mbali kinyume na sisi na asingejitahidi kutufuatilia ili tumrudie yeye. Tofauti iliyopo kati yetu na mataifa ya kipagani ni kwa mfano huu: Dhoruba ya mawimbi ya Tsunami iliyopiga pande za Kusini-mashariki mwa Asia, iliangamiza watu waliokuwa wanaabudu miungu ya uwongo. Lile kwa wao halikuwa ni onyo kama alivyofanya kwetu sisi. Yale yalikuwa ni maangamizo. Mungu hakuweka sababu fulani ili kufanya jambo lile litokee, bali aliugeuza uso wake mbali na watu hawa ambao wamekuwa wamemuacha na kuitumikia miungu mingine kwa muda mrefu. Walikuwa na uhuru wa kuchagua kuishi ama kutoishi. Kama Mungu akiugeuza uso wake mbali na watu na kuacha kuwapa ulinzi, basi maafa ndio yatakuwa ni matokeo ya hali yake hii ya kutoongoza kila kitu. Basi maumbile ya asili huchukua hatua ya kawaida yenye kuleta maafa. Hivyo basi haitawezekana kuepusha kutokea maafa na uharibifu visitukumbe pasipo fanyika uangalifu ama matengenezo ya mara kwa mara. Nyumba zetu, milki za ndoa zetu, milima yetu mikubwa na mizuri na ardhi tunavyoviona vikiharibika kila mara kwa vikimomonyoka na kutepeta na vikikumbwa na madhara mengine mengi ya kimaumbile. Iwapo kama kusingekuweko na ushawishi wa mara kwa mara wa kusaidiwa na viumbe vingine nje ya asli yake basi vingekoma kuendelea kwake kuishi.

Tumebarikiwa na Mungu mwenye rehema kuu ambaye anaungalia na kuutunza ulimwengu wetu pamoja na sisi ikiwa tu kama tutamwamini na kuzitii amri na sheria zake. Ni uhuru mkubwa na mpana tunapokuwa tunamuabudu kwa hiyari yetu, yeye aliye Mungu wa pekee na wa kweli. Hapo ndipo tutaweza kuponywa na kuwekwa huru na mashambulizi ya maradi, maafa na tauni za kila namna.

REJEA KWENYE UKURASA MKUU