Maneno ya Ukweli

Kama yalivyofunuliwa kwenye Maandiko Matakatifu

Itifaki ya Somo

kuhusu :

Mungu

Mwanadamu

Mwokozi wa Mwanadamu, Bwana Yesu Kristo

Ufalme Wake Unaokuja

Ukamilifu Usioharibika wa Watu Wake

na

Kuharibiwa kwa Watendadhambi

Imeandaliwa na

Harry Goekler,

E.L. Macy,

G.G. Landry,

na

James Mattison

Yakachapishwa kwa ajili ya

Shirika la Jumuia ya Vijana la Waberoya wa Kusini wa Kanisa la Mungu


Maneno ya Ukweli

Kama yalivyofunuliwa kwenye Maandiko Matakatifu

Yakachapishwa kwa ajili ya

Shirika la Jumuia ya Vijana

La Waberoya wa Kusini wa Kanisa la Mungu

ASILI YA JINA "WABEROYA"

"Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya, Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo." – Matendo 17: 10, 11.

KAULI-MBIU YETU:

Chunguza Maandiko Matakatifu Kilasiku

MSIMAMO WETU:

Tunasisitizia Umoja, Ukweli, Na Utakatifu

Jumuia ya Waberoya ya Kusini ilianzishwa kwenye kongamano la viwanja vya huko Pidcoke karibu na Gatesville, Texas, siku ya Ijumaa, Tarehe 16, Julai 1954, na kundi mchanganyiko la vijana waumini wa Kanisa la Mungu na viongozi wao kutoka Texas na Lousiana.

Dhumuni kuu lilikuwa ni kuwaunganisha vijana wa majimbo haya mawili na majimbo jirani kwa kutumia kongamano la kila mwaka la vijana la Waberoya wa Kkusini na Gazeti la kila mwezi la Waberoya wa Kusini lijulikanalo kama Southern Berean Newspaper.

Mahudumu husika walikuwa ni Ndugu Bros. D.A. Jones, E.L. Macy, Gordon Landry, na

James Mattison.

Kijitabu hiki cha mafundisho kimechapishwa kama mradi mkakati na Jumuia ya Kusini ya Waberoya.


Biblia, Neno la Mungu – Kwa Wokovu Wetu

Soma Biblia

MUNGU WETU, BWANA WA MAJESHI

Mungu Mwenyezi ----- Mungu Mmoja

Muumba wa Vitu Vyote

Baba

Mungu wa Yesu

Baba wa Yesu

Asili ya Yehova na Tabia Zake

Mpango Wake Kwa Zama Mbalimbali

ASILI YA MWANADAMU, UFUFUKO WAKE, IZIMA WAKE WA MILELE, NA KUANGAMIZWA KWAO WATENDA DHAMBI

Mwanadamu Aliumbwa Akiwa Hana Dhambi

Dhambi Zilimgharimu Mwanadamu "Maisha ya Milele"

Mwanadamu ni wa Ardhini --- Mavumbi, na Sio Roho

Pumzi ya Mungu Huwapa Uhai Watu Hawa Walio Mavumbi

Mwanadamu Huyarudia Mavumbi ya Ardhi

Pumzi ya Mungu ya Uzima (Roho) Hurudi kwa Mungu Wakati Mwanadamu Akiyarudia Mavumbi

Kifo Kinaitwa "KULALA"

Mwanadamu Huchakaa, Ndiyo Maana, Hatimayake Anakufa

Mwanadamu Hakupewa Nafsi Hai, Bali Alifanyika Kuwa Nafsi Hai

Nafsi ni Utu Halisi, au Uzima

Nafsi Huchakaa na Kufa

Nafsi ya Kristo Ilikufa

Nafsi Huenda Kaburini Akifa

Maana za Neno "ROHO"

Maana ya jumla: ni msukumo usioonekana, uweza au ushawishi

Roho ya Mwanadamu

Kifo ni Matokeo ya Dhambi

Je, Ni Nani Basi Mwenye Mwili Usioharibika?

Watakatifu Waliokufa Hawapo Mbinguni

Kutakuwa na Ufufuo wa Wafu Wote

Watakatifu Watapewa Mwili Usiochakaa Wakati Kristo Atakapokuja, Kwa Ufufuo wa Kwanza wa Wafu

Wafu waliosalia Watafufuliwa Kwenye Ufufuo wa Mwisho, Baada ya Miaka Elfu

Watendadhambi Watahukumiwa na Kutupwa Kwenye Ziwa la Moto, Hii Ndiyo Mauti ya Pili

Uzima wa Milele Una Masharti Yake. Watendadhambi Hawataishi Milele

Watendadhambi Watatokomezwa

Watendadhambi Watakatiliwa Mbali

Watendadhambi Watatoweshwa Wote

Watendadhambi Wataangamizwa Kabisa

Watendadhambi Watachomwa na Kuunguzwa Kabisa

Kaburi Kuzimuni(Shimoni)

Kaburi Kuzimuni, Kuliendelezwa Kuitwa (Hades)

Ziwa la Moto Kuzimuni ----- Hatimaye

MWOKOZI WA MWANADAMU, BWANA WETU YESU KRISTO

Yesu, Mwana wa Mungu

Yesu -----Alitumwa Toka kwa Mungu Kuokoa Waliopotea

Yesu -----Alitumwa Kumkomboa Mwanadamu Toka Dhambini

Yesu Mwenyewe Hakuwa na Dhambi

Akiwa Hana Dhambi, Alifanyika Kuwa ni Dhabihu Kamilifu

Yesu Kristo ni Mwokozi Pekee

Yesu Kristo Alikufa, Alizikwa, Akafufuka

Na Sasa Anatuombea Mbinguni

Kristo Anakuja Tena ----- Mara ya Pili, Yeye Mwenyewe na Ataonekana, Kwa Nguvu na Utukufu

Mambo Haya Yamhusuyo Yesu Kristo Ni Miongoni Mwa Injili (Ionyeshayo Jinsi Dhambi Inavyoweza Kusamehewa)

UFALME WA MILELE WA MUNGU

Sehemu Nyingine ya Injili Kuhusiana na Ufalme wa Mungu (Makao Yajayo ya Milele ya Waliokombolewa, Wokovu Wetu Utakapokamilika)

Ufalme wa Mungu Bado ni Kwa Siku za Zinazokuja Mbele

Utakuwa Hapahapa Duniani

Nchi Itadumu na Kuwepo Milele

Nchi Itakombolewa Kutokakana na Laana, Kufanywa Upya na Kutukuka

Nchi, Urithi wa Milele wa Watakatifu

Urithi wa Nchi Uliahidiwa Kupitia Agano la Ibrahimu

Kristo Atatawala Akiwa ni Mfalme wa Dunia Hii Kwa Kipindi Cha Miaka Elfu, na Atawaseta Maadui Zake Chini ya Miguu Yake

Jambo Hili Litatilimiliza Agano la Daudi

Watakatifu Wake Kristo Watatawala Pamoja Naye

Taifa la Israeli Litapewa Milki Yake

Mitume Kumi na Mbili Watazihukumu Kabila Kumi na Mbili ya Israeli

Makao Makuu ya Ulimwengu ----- Yerusalemu

Mataifa Watakaokuwepo (Kipindi Hiki Cha Miaka Elfu) Watajifunza Njia za Mungu

Adui wa Mwisho ----- Mauti ----- Ataharibiwa

Kristo Atakabidhi Ufalme Mkamilifu kwa Baba Yake, Ili Mungu Awe Yote Katika Yote

Ishara Zinazoashiria Kuwa Kurudi Kwa Kristo Kupo Karibu

Walimu wa Uwongo

Ukengeufu

Ishara za Mbinguni

Ishara za Duniani

Kurudi Kwa Waisraeli Kwenye Ardhi ya Palestina

Israeli, Kuwa Taifa Tena Katika Ardhi ya Palestina, Kuchangamanywa

Watu wa Nyumbani Mwake Mungu

Jina la Kanisa la Kweli

TUNAPASWA KUFANYA NINI KWA WOKOVU "MKUU"

Kuwa na Imani, Kuamini

Tubu

Ubatizwe

Ishi Maisha Matakatifu – Ikulie Neema na Kumjua Kristo


"TENA MTAIFAHAMU KWELI,

NAYO HIYO KWELI ITWAWAWEKA HURU"

- YESU, KATIKA YOHANA 8:32

Biblia, Neno la Mungu – Kwa Wokovu Wetu

2 Petro 1:21 ----- Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya wanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Yakobo 1:18 ----- Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli.

Yakobo 1:21 ----- neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuokoa roho zenu.

Yohana 6:63 ----- maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.

Yohana 6:68 ----- Wewe unayo maneno ya uzima.

Yohana 12:48 -----neno hilo nililolinena … litakalomhukumu siku ya mwisho.

Warumi 1:16 ----- injili,... ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye.

2 Wathesalonike 2:10 ----- kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.

1 Petro 1:25 ----- Bali neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

Soma Biblia

2 Timotheo 2:15 ----- ukilitumia kwa halali neno la kweli.

Yohana 5:39 ----- Mwayachunguza maandiko.

Matendo 17:11 ----- wakayachunguza maandiko kila siku.

MUNGU WETU, BWANA WA MAJESHI

Mungu Mwenyezi ----- Mungu Mmoja

Kumbukumbu la Torati 4:35 ----- BWANA ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye.

Kumbukumbu la Torati 6:4 ----- Skia, Ee Israeli: BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja.

Waefeso 4:6 ----- Mungu mmoja.

1 Wakorintho 8:6 ----- lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu.

Isaya 44:6 ----- BWANA asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.

Isaya 44:8 ----- je! yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.

Muumba wa Vitu Vyote

Mwanzo 1:1 ----- Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Ayubu 9:8 ----- Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu.

Zaburi 95:6 ----- Tupige magoti mbelet za BWANA aliyetuumba.

Isaya 40:28 ----- Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia.

Isaya 44:24 ----- Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; nienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?

Isaya 45:12 ----- Maana nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake.

Isaya 45:18 ----- Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, aseme hivi; Yeye ni Mungu, ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.

Marko 13:19 ----- kuumbwa alipoumba Mungu.

Baba

Zaburi 103:13 ----- Kama vile baba awarudivyo watoto wake, Ndivyo BWANA awarudivyo wamchao.

Mathayo 6:9 ----- Baba yetu uliye mbinguni.

Mathayo 6:14 ----- Baba yenu wa Mbinguni.

Warumi 15:6 ----- kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

1 Petro 1:17 ----- mnamwita Baba.

Mungu wa Yesu

Yohana 20:17 ----- Nimepaa kwenda kwa Baba… kwa Mungu wangu.

Waefeso 1:17 ----- Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Ufunuo wa Yohana 3:12 ----- Mungu wangu.

Baba wa Yesu

Mathayo 3:17 ----- Na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu.

Mathayo 7:21 ----- yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

Marko 1:11 ----- Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Luka 2:49 ----- Hakujuua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?

Luka 9:35 ----- Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye.

Yohana 11:41 ----- Basi wakaliondoa lile jiwe, Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa unanisikia.

Asili ya Yehova na Tabia Zake

Isaya 42:8 ----- Mimi ni BWANA (Yehova); ndilo jina langu;

Isaia 46:9, 10 ----- maana Mimi ni Mungu, wala hapana mwingine … nitangazaye mwisho tangu mwanzo.

Isaya 40:13, 14 ----- Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza .… maarifa?

Zaburi 139:7, 8 ----- Niende wapi nijiepushe na roho yako? … mbinguni, wewe uko; … kuzimu (sheol, kaburini) …, Wewe uko.

1 Timotheo 1:17 ----- Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, heshima na utukufu milele na milele.

Yohana 3:16 ----- Mungu aliupenda ulimwengu.

Isaya 45:21 ----- Mungu mwenye haki.

Yakobo 5:11 ----- Bwana ni mwingi wa rehema.

Zaburi 25:10 ----- Njia zote za BWANA ni fadili na kweli, Kwao walishikao agano lake na ushuhuda wake.

Mpango Wake Kwa Zama Mbalimbali

Matendo 15:18 ----- Asema Bwana, ajulishaye hayo yangu milele.

Isaya 46:10 ----- Nitangazaye mwisho tangu mwanzo, … nitatenda mapenzi yangu yote.

Isaya 45:18 ----- Mungu; ndiye aliyeiumba dunia … aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu.

Yohana 3:16 ----- Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Habakuki 2:14 ------ Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari.

Isaya 65:17 ----- Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya.

2 Petro 3:13 ----- tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

Ufunuo wa Yohana 21:3 ----- Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

1 Wakorintho 15:28 ----- ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake … ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

ASILI YA MWANADAMU, UFUFUKO WAKE, IZIMA WAKE WA MILELE, NA KUANGAMIZWA KWAO WATENDA DHAMBI

Mwanadamu Aliumbwa Akiwa Hana Dhambi

Mwanzo 2:7 ----- BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Mwanzo 1:31 ----- Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.

Mwanzo 2:16, 17 ----- BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Dhambi Zilimgharimu Mwanadamu "Maisha ya Milele"

Mwanzo 3:11 ----- Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?

Mwanzo 3:12,13 ----- Nikala [mwanaume]. Nikala [mwanamke]

Mwanzo 3:22, 23 ----- asije ... akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; kwa hiyo BWANA, Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni.

Mwanzo 3:24 ----- Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi … na upanga wa moto … kuilinda njia ya mti wa uzima.

Warumi 5:12 ----- kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; … hivyo mauti ikawafikia watu wote.

Warumi 3:23 ----- Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu

Warumi 6:23 ----- Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.

Mwanadamu ni wa Ardhini --- Mavumbi, na Sio Roho

Mwanzo 2:7 ----- BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi.

Mwanzo 3:19 ----- kwa maana u mavumbi wewe (ardhi), nawe mavumbini utarudi.

Mwanzo 18:27 ----- Nami ni mavumbi na majivu tu.

Zaburi 103:14 ----- Kwa maana, Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.

Yohana 3:31 ----- Yeye aliye wa dunia, asili yake ni wa dunia.

I Wakorintho 15:47 ----- Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo.

I Wakorintho 15:48 ----- Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo..

Pumzi ya Mungu Huwapa Uhai Watu Hawa Walio Mavumbi

Mwanzo 2:7 ----- pumzi ya uhai.

Mwanzo 7:22 ----- kila kitu chenye ya roho ya uhai … kikafa.

Ayubu 27:3 ----- roho ya Mungu I katika pua yangu.

Ayubu 33:4 ----- Roho ya Mungu imeniumba, na pumzi ya Mungu hunipa uhai.

Ayubu 34:14 ----- roho yake na pumzi yake.

Isaya 2:22 ----- mwanadamu ambaye pumzi yake I katika mianzi ya pua yake.

Isaya 42:5 ----- yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake

Danieli 5:23 ----- Mungu yule, ambaye pumzi yako I mkononi mwake.

Zaburi 104:29 ----- Waiondoa pumzi yao, wanaokufa, Na kuyarudia mavumbi yao.

Mhubiri 3:19 ----- wote wanayo pumzi moja.

Ezekieli 37:5, 6, 8, 10 ----- kutia pumzi ndani yenu.

Matendo 17:25 ----- aliyewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.

Yoshua 10:40 ----- akawaharibu kabisa wote waliokuwa wavuta pumzi. (Wakti hii ilipotokea, "roho" hizo ziliangamizwa, aya ya. 39).

Mwanadamu Huyarudia Mavumbi ya Ardhi

Mwanzo 3:19 ----- u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

Ayubu 34: 15 ----- wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.

Ayubu 40:13 ----- Wafiche mavumbini pamoja.

Zaburi 104:29 ----- wanakufa, Na kuyarudia mavumbi.

Zaburi 146:4 ----- hurudia udongo wake.

Mhubiri 3:20 ----- wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.

Mhubiri 12:7 ----- Nayo mavumbi huirudia nchi kama yalivyokuwa.

Pumzi ya Mungu ya Uzima (Roho) Hurudi kwa Mungu Wakati Mwanadamu Akiyarudia Mavumbi

Mhubiri 12:7 ----- Nayo mavumbi huirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho humrudia Mungu aliyeitoa.

Mwanzo 2:7 ----- BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Ayubu 34:14, 15 ----- Kama akimwekea mtu moyo wake, akijikusanyia roho yake na pumzi zake.

Zaburi 104:29 ----- Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao.

Zaburi 146:4 ----- Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake.

Kifo Kinaitwa "KULALA"

Kumbukumbu la Torati 31:16 ------ Musa, Angalia, wewe utalala na baba zako.

1 Wafalme 2: 10 ----- Basi Daudi akalala na baba zake, akazikwa

1 Wafalme 11:43 ----- Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa

Ayubu 7:21 ----- sasa nitalala mavumbini.

Ayubu 14.12 ----- hawatainuka, Wala kuamshwa usingizini.

Zaburi 13:3 ----- Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.

Danieli 12:2 ----- Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi.

Yohana 11: 11, 14 ----- Rafiki yetu Lazaro amelala … Lazaro amekufa.

Matendo 7:60 ----- Akisha kusema haya, akalala.

Matendo 13:36 -----Kwa maana Daudi, ... alilala ... akaona uharibifu.

1 Wakorintho 15:20 ----- Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, llimbuko lao waliolala.

1 Wathesalonike 4:13 ----- hatutaki msijue habari zao waliolala.

1 Wathesalonike 4:14 ----- waliolala katika Yesu.

Mwanadamu Huchakaa, Ndiyo Maana, Hatimayake Anakufa

Ayubu 4:17 ----- Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu?

Ayubu 14:10 ----- Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia.

Zaburi 89:48 ----- Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti?

Yohana 6:49 ----- Baba zenu walikula mana … wakafa.

Yohana 8:52 ----- Ibrahimu amekufa, na manabii.

Warumi 6:12 ----- Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti.

Waebrania 9:27 ----- Na kama vile watu walivyowekewa kufa.

Mwanadamu Hakupewa Nafsi Hai, Bali Alifanyika Kuwa Nafsi Hai

Mwanzo 2:7 ----- BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

1 Wakorintho 15:45 -----Ndivyo iivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai.

Nafsi ni Utu Halisi, au Uzima

Mwanzo 46:26 ----- Nafsi zote zilizokuja pamoja na Yakobo mpaka Misri … walikuwa sitini na sita.

Kutoka 12:19 ----- Nafsi hiyo itakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli.

Hesabu 15:27 ----- Tena kama mtu mmoja akifanya dhambi pasipo kujua

Matendo 2:41 ----- na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

Matendo 2:43 ----- Kila mtu akaingiwa na hofu!

Matendo 27:37 ----- Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu mia mbili na sabini na sita.

1 Petro 3:20 ----- ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.

Marko 8:35-37 ----- Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakaye iangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyo ataisalimisha. Kwa kuwa, itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake

Nafsi Huchakaa na Kufa

Yoshua 10:35 ----- na wote pia waliokuwamo ndani yake wakaangamizwa kabisa.

Yoshua 11:11 ----- Nao wakawapiga wote waliokuwamo ndani ya Hazori kwa makali ya upanga, wakawaangamiza kabisa.

Zaburi 22:29 ----- yeye asiyeweza kuihuisha nafsi yake.

Zaburi 78:50 ----- Wala hakuziepusha roho zao na mauti.

Zaburi 89:48 ----- Atakayeiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?

Zaburi 119:175 ----- Nafsi yangu na iishi, ipate kukusifu.

Ezekieli 18:4 ----- roho ile itendayo dhambi, itakufa.

Ezekieli 22:27 ----- Wakuu wake ... huharibu roho za watu, wapate faida kwa njia isiyo halali.

Yakobo 5:20 ----- yeye amrejezaye mwenye dhambi … ataokoa roho na mauti.

Ufunuo wa Yohana 16:3 ----- na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.

Nafsi ya Kristo Ilikufa

Isaya 53:10 ----- Utakapofanya roho yako dhabihu ya dhambi.

Isaya 53:12 ----- alimwaga nafsi yake hata kufa.

Mathayo 26:38 ----- Roho yangu ina huzuni nyingi, kiasi cha kufa.

Marko 10:45 ----- Mwana wa Adamu naye hakuja ..., bali kutumika, na kuitoa nafsi yake iwe fidia kwa wengi.

Matendo 2:27 ----- Kwa maana hakuiacha roho yangu katika kuzimu.

Matendo 2:31 ----- kufufuka kwake Kristo, na kwamba roho yake haikuachwa kuzimu.

Warumi 5:6 ----- Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.

1 Wakorintho 15:3 ----- Krist alikufa kwa ajili ya dhambi zetu.

Ufunuo wa Yohana 1:18 -----nami nilikuwa nimekufa.

Nafsi Huenda Kaburini Akifa

Ayubu 33:22 ----- Naam, nafsi yake inakaribia shimoni.

Zaburi 16:10 ----- Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu [sheol, kaburi].

Zaburi 49:15 ----- Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu.

Zaburi 89:48 ----- Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?

Isaya 38:17 ----- kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu.

Yeremia 18:20 ----- wamenichimbia nafsi yangu shimo.

Matendo 2:27 ----- Kwa maana hataiacha roho yangu katika kuzimu [kuzimuni, kaburini].

Matendo 2:31 ----- Yeye ... alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haitaachwa kuzimu, .

Maana za Neno "ROHO"

Maana ya jumla: ni msukumo usioonekana, uweza au ushawishi

1.Pumzi ya Uhai.

Mwanzo 6:17 ----- Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kiIa kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, … kila kilichoko duniani kitakufa.

Mwanzo 7:15 ----- Waliingia katika Safina alimo Nuhu, wawili wawili, na kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake.

Mwanzo 7:22 ----- Kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kitambaacho katika nchi kavu.

Mhubiri 12:7 ----- Nayo mavumbi huirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho humrudia Mungu aliyeitoa.

2. Upepo (hali ya hewa ya anga, hali ya kimazingira).

Mwanzo 3:8 ----- Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga.

Mwanzo 8:1 ----- Mungu akavumisha upepo juu ya nchi.

1 Wafalme 18:45 ----- mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu ya upepo.

Zaburi 1:4 ----- ni kama makapi yapeperushwavyo na upepo.

Zaburi 55:8 ----- Ningefanya haraka kuzikimbia, Dhoruba na tufani.

Danieli 2:35 ----- upepo ukayapeperusha.

Yona 1:4 ----- Lakini BWANA lituma upepo mkuu baharini.

3. Uweza au mvuto toka kwa Mungu.

Mwanzo 1:2 ----- Roho [ruach] ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Mathayo 3:16 ----- akamwona Roho [Kwa Kiyunani ni "pneuma" yenye maana sawa na Kiebrania ruach] wa Mungu akishuka. (Kumbuka: nguvu hii toka kwa Mungu imetendakazi kwa namna mbalimbali kupitia kwa nyakati mbalimbali)

4. Mahala pa Utashi, ama hisia (iitwayo roho "njema"au "mbaya").

Kumbukumbu la Torati 34:9 ----- roho ya hekima.

Hesabu 5:14 ----- roho ya wivu.

1 Samweli 1:15 ----- roho ya huzuni.

Ayubu 20:3 ----- roho ya ufahamu.

Mithali 16:18 ----- roho yenye kutakabari.

Isaya 11:2 ----- roho ya shauri na uweza.

Ufunuo wa Yohana 18:2 ----- roho chafu.

5. Uhuisho, utiisho, nguvu.

Waamuzi 15:19 ----- naye alipokwisha kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika.

1 Samweli 30:12 ----- naye akiisha kula, roho yake ikamrudia.

1 Wafalme 10:5 ----- roho yake ilizimia. (Kumbuka: maneno haya "nafsi yanye kufa" au "roho yenye kufa" hayakutumika kwenye Biblia).

Roho ya Mwanadamu

Ayubu 32:8 ----- Lakini imo roho ndani ya mwanadamu.

Ayubu 27:3 ----- roho ya Mungu I katika pua yangu.

Ayubu 33:4 ----- Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai.

Ayubu 34:14, 15 ----- Kama alimwekea mtu uhai wake, aIijikusanya roho yake na pumzi yake; Wenye mwili wote wataangamia pamoja, Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.

Hesabu 16:22 ----- Mungu wa wote wenye mwili.

Mhubiri 12:7 ----- Nayo mavumbi huirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho humrudia Mungu aliyeitoa.

Yakobo 2:26 ----- mwili pasipo horo umekufa.

Kifo ni Matokeo ya Dhambi

Mwanzo 2:17 ----- kwa maana siku utakayokula matunda ya mti huo utakufa hakika

Warumi 1:32 ----- wayatendao hayo wamwstahili mauti.

Warumi 5:12 ----- kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti.

Warumi 5:17 ----- kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja.

Warumi 6:16 ----- kuwa watumwa wake katika kumtii … utumishi wa dhambi uletao mauti.

Warumi 6:23 -----mshahara wa dhambi ni e mauti.

Je, Ni Nani Basi Mwenye Mwili Usioharibika?

1 Timotheo 1: 17 ----- Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu.

1 Timotheo 6:15,16 ----- Bwana wa mabwana; ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti.

Yohana 5:26 ----- Maana kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake, viyo hivyo alimpa Mwana kuwa na uzima nafsini mwake

Warumi 6:9 ----- tukijua kwamba Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.

Ufunuo wa Yohana 1:18 ----- naimi nalikuwa nimekufa na tazama, ni hai hata milele.

Watakatifu Waliokufa Hawapo Mbinguni

Matendo 2:34 ----- Maana Daudi hakupanda mbinguni.

Yohana 3:13 ----- Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni [ila Mwana wa Adamu].

Yohana 7:33, 34 ----- nami nilipo ninyi hamwezi kuja.

Yohana 13:33 ----- na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.

1 Timotheo 6:16 ----- nuru isiyoweza kukaribiwa.

Mithali 11:31 ----- mwenye haki atalipwa duniani.

Mathayo 5:5 ----- wapole ... watairithi nchi.

Waebrania 11:39,40 ----- Na watu hawa wote wakisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.

Kutakuwa na Ufufuo wa Wafu Wote

Zaburi 22:29 ----- humwinamia wote washukao mavumbini.

Isaya 26:19 ----- ardhi itawatoa waliokufa.

Isaya 26:21 ----- ardhi nayo itafunua damu yake … haitawafunika tena watu wake waliouawa.

Yeremia 31:16 ----- watakuja tena toka nchi ya adui.

Hosea 13:14 -----Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti.

Yohana 5:28, 29 ----- watu wote waliomo makaburini wataitikia sauti yake. Nao watatoka.

Matendo 24:15 ----- kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.

Matendo 26:8 ----- Kwa nini ... kuwa ni neno lisilosadikika, kwamba Mungu awafufua wafu?

1 Wakorintho 15:22 ----- katika Adamu wote wanakufa ... katika Kristo wote wanahuishwa.

2 Wakorintho 5:10 ----- Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo; ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyoyatenda …, kwamba ni mema ama mabaya.

Ufunuo wa Yohana 20:4, 5 ----- wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.

Watakatifu Watapewa Mwili Usiochakaa Wakati Kristo Atakapokuja, Kwa Ufufuo wa Kwanza wa Wafu

Ufunuo wa Yohana 20:6 ----- Heri na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu.

Ayubu 14:14 ----- Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningemngoja siku zote za vita vyangu, Hata kufunguliwa kwangu kutimie.

Zaburi 17:15 ----- Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.

Marko 10:30 ----- na katika ulimwengu ujao uzima wa melele.

Luka 18:30 ----- katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

Luka 20:35,36 ----- lakini wao wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, … wala hawawezi kufa tena.

Yohana 6:40 -----awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Warumi 2:7 ----- Wale ambao … wanatafuta utukufu na heshima na kuto kuharibika, watapewa [Mungu atawatunukia] uzima wa milele.

Warumi 8:11 ----- yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yetu.

I Wakorintho 15:42 ----- Kadhalika na kiyama ya wafu.

I Wakorintho 15:43 ----- hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari, … kufufuliwa katika nguvu.

I Wakorintho 15:44 ----- kufufuliwa mwili wa roho.

I Wakorintho 15:49 ----- Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tumeichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

I Wakorintho 15:52 ----- wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

I Wakorintho 15:53 ----- huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika.

I Wakorintho 15:54 ----- Basi ... uharibikao utakapovaa kutoharibika.

Wafilipi 3:20, 21 ----- Kristo ... atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu.

Waebrania 11:35 ----- wengine waliumizwa … ili wapate ufufuo ulio bora.

1 Yohana 3:2 ----- atakapodhihirishwa, tutafanana naye.

Wafu waliosalia Watafufuliwa Kwenye Ufufuo wa Mwisho, Baada ya Miaka Elfu

Ufunuo wa Yohana 20:5 ----- Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie hiyo miaka elfu.

Danieli 12:2 ----- Tena, wengi wa hao … wataamka … wengine aibu na kudharauliwa milele.

Yohana 5:28, 29 ----- watu wote waliomo makaburini … Nao watatoka; … wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.

Matendo 24:15 ----- kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasiohaki pia.

2 Wakorintho 5:10 ----- Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyoyatenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.

Watendadhambi Watahukumiwa na Kutupwa Kwenye Ziwa la Moto, Hii Ndiyo Mauti ya Pili

Ayubu 21:30 ----- Kwamba waovu huachiliwa katika siku ya msiba?

Mathayo 12:3 6 ----- Kila neno … watatoa hesabu hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.

Mathayo 13:42 ----- na kuwatupa katika tanuru ya moto.

Yohana 12:48 ----- Yeye anikataaye mimi, asiyekubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo ninaloninena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

Warumi 2:5, 6 ----- Mungu ... atakayemlipa kwa kadiri ya matendo yake.

Warumi 6:23 ----- Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.

Wagalatia 6:7 ----- cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Wagalatia 6:8 ----- yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu.

2 Petro 2:9 ----- kuwaweka wasi haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu.

Ufunuo wa Yohana 2:11 -----mauti ya pili.

Ufunuo wa Yohana 20:12 ----- Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa, … sawa sawa na matendo yao.

Ufunuo wa Yohana 20:14 ----- ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili.

Ufunuo wa Yohana 20:15 -----Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Ufunuo wa Yohana 21:8 ----- sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Uzima wa Milele Una Masharti Yake. Watendadhambi Hawataishi Milele

Yohana 3:16 ----- kila amwaminiye aipotee, bali awe … uzima wa milele.

Mithali 15:10 ----- Naye achukiaye kukemewa atakufa.

Mithali 19:16 ----- Bali yeye asiyeziangalia njia zake [Mungu] atakufa.

Ezekieli 18:23 ----- Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu muovu?

Mathayo 19:16 ----- Mwalimu, nitende jambo gani ... ili nipate uzima wa milele?

Mathayo 19:17 ----- ukitaka kuingia katika uzima, zishie amri.

Yohana 3:36 - ----asiyemwamini Mwana hataona uzima.

Yohana 6:50 - ----Hiki chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akila asife.

Yohana 6:51 ----- mtu akila chakula hiki, ataishi milele.

Yohana 6:53 ----- Msipokula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hmna uzima ndani yenu.

Yohana 20:31 ----- na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina lake.

Warumi 6:21 ----- Kwa maana mwisho wa hayo yote ni mauti.

Warumi 8:13 ----- Kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa:

1 Yohana 3:15 ----- kila mwuuaji hana uzima wa milele.

1 Yohana 2:25 -----Na hii ndio ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele.

1 Yohana 5:11 ----- Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu unao katika Mwanawe.

1 Yohana 5:12 ----- Yeye aliyenaye Mwana, anao huo uzima; asiyenaye Mwana wa Mungu hana huo uzima.

Ufunuo wa Yohana 2:11 ----- Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

Ufunuo wa Yohana 20:6 ----- juu ya hao mauti ya pili haina nguvu.

Ufunuo wa Yohana 21:8 ----- [Watendadhambi] sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Watendadhambi Watatokomezwa

Zaburi 37:20 ----- watapotea, … kama moshi watatoweka.

Zaburi 59:13 ----- Uwatokomeze kwa hasira, Uwakomeshe watoweke.

Zaburi 104:35 ----- Wenyedhambi waangamizwe katika nchi, Watendao ubaya wasiwepo tena.

Isaya 1:28 ----- nao wamwachao BWANA watateketezwa.

Watendadhambi Watakatiliwa Mbali

Zaburi 12:3 ----- BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza,

Zaburi 37:9 ----- Maana watenda mabaya wataharibiwa.

Zaburi 37:22 -----Nao waliolaaniwa na yeye wataharibiwa.

Zaburi 37:28 ----- mzao wa wasio haki utaharibiwa.

Zaburi 37:34 ----- Wasio haki watakapo haribiwa utawaona.

Zaburi 37:38 ----- Wasio haki mwisho wao wataharibiwa.

Zaburi 104:35 ----- Watendao ubaya wasiwepo tena.

Mithali 2:22 ----- Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang’olewa.

Watendadhambi Watatoweshwa Wote

Ayubu 20:7 ----- Hata hivyo ataangamia milelet kama mavi yake mwenyewe.

Zaburi 1:6 ----- Bali njia ya wasio haki itapotea.

Zaburi 37.20 ----- Bali wasio haki watapotea.

Zaburi 73:27 ----- wajitengao nawe watapotea.

Mithali 19:9 ----- Shahidi wa uwongo … Naye asemaye uongo ataangamia.

Luka 13:3 ----- msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

Yohana 3:15, 16 ----- ili kila mtu amwaminiye asipotee.

Yohana 10:27, 28 ----- Kondoo wangu waisikia sauti yangu; … Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe.

Matendo 13:41 ----- Tazameni, enyi mnaodharau, kastaajabuni, mkatoweke.

Warumi 2:12 ----- Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria.

1 Wakorintho 1:18----- Kwa sababu neno la msalaba kwa wanaopotea ni upuzi.

2 Wakorintho 2:15 ----- Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu … na katika wao wanaopotea.

2 Wathesalonike 2:10 ----- na katika maganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea.

2 Petro 2:12 ----- wataangamizwa kabisa maangamizo yao

Watendadhambi Wataangamizwa Kabisa

Ayubu 31:3 ----- Je! Sio msiba kwa wasio haki?

Zaburi 37:38 ----- Wakosaji wataangamizwa pamoja.

Zaburi 92:7 ----- kusudi waangamizwe milele.

Zaburi 145:20 ----- Na wote wasio haki wataangamizwa.

Mithali 10:29 ----- Bali ni uharibifu kwao watendao maovu.

Mithali 13:13 ----- Kila ajitengaye na neno hujiletea uharibifu.

Mithali 21:15 ----- uharibifu kwao watendao maovu.

Mithali 31:8 ----- watu wote walioachwa peke yao.

Isaya 1:28 ----- Lakini kuharibika kwao wakosao nao wenye dhambi kutatokea wakati mmoja.

Isaya 13:9 ----- na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake [kwenye nchi].

Mathayo 7:13 ----- na njia ni pana iendayo upotevuni.

Matendo 3:23 ----- kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.

Warumi 9:22 ----- vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu.

Wafilipi 3:18, 19 ----- adui wa msalaba wa Kristo: mwisho wao ni uharibifu.

2 Wathesalonke 1:9 ----- watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana.

Waebrania 2:14 ----- amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Ibilisi

2 Petro 2:1 ----- wakimkana hata Bwana … wakijiletea uharibifu usiokawia.

2 Petro 3:16 ----- watu … huyapotoa … maandiko mengine kwa uvunifu wao wenyewe.

Watendadhambi Watachomwa na Kuunguzwa Kabisa

Zaburi 11:6 ----- Awanyeshee wasio haki mitego, Moto wa kiberiti na upepo wa hari.

Zaburi 21:9 ----- Utakapofanya kama tanuru … Na moto utawala.

Malaki 4:1 ----- siku ile inakuja inawaka kama tanuru; … itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.

Malaki 4:3 ----- watakuwa majivu chini … nyayo za miguu yenu.

Mathayo 3:12 ----- bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.

Mathayo 13:41, 42 ----- watakisanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote na hao watendao maasi … na kuwatupa katika tanuru ya moto.

Yohana 15:6 ----- kama tawi … kuyatupa motoni yakateketea.

Waebrania 10:27 ----- kuitazamia hukumu yenye kutisha.

2 Petro 3:7 ----- zimewekwa akiba kwa moto … zikilindwa hata siku ya hukumu, na kuangamizwa kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

Ufunuo wa Yohana 20:15 ----- hakuonekana ... kitabu cha uzima, alitupwa kwenye lile ziwa la moto.

Ufunuo wa Yohana 21:8 ----- [Waovu] sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Kaburi Kuzimuni

Sheol, ni neno la Kiebrania katika Agano la Kale lenye maana ya mahali pa wafu, limetafsiriwa kuwa kaburi na limeandikwa kaburi mara 31, kuzimuni mara 31 na shimoni mara 3.

1. Wote wawili yaani watakatifu na waovu huenda huko sheol wanapokufa.

Zaburi 16: 10 ----- Maana hutakuacha kuzimu nafsi yangu [sheol].

Zaburi 89:48 ----- Ni mwanaume gain atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu [sheol]?

2. Ayubu, mtu mwenye haki mcha Mungu, alipenda afichwe kwenye hiyo sheol hadi hapo ghadhabu ya Mungu itakapopita.

Ayubu 14:13 ----- Laiti wangenificha kuzimuni [sheol] ... hata ghadhabu zako zitakapopita.

3 . Yakobo, mtu atakayekuwepo katika Ufalme wa Mungu , alisema kuwa alikuwa anashukia chini kuzimuni kumuombolezea motto wake.

Mwanzo 37:35 -----nitamshukia mwanangu nikisikitika, hata kuzimu [sheol].

4. Hezekia, muda mfupi tu baada ya Mungu kujibu maombi yake, alisema kwamba alikuwa anaelekea kwenye malango ya kuzimu.

Isaya 38: 10 ----- Nalisema katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu [sheol]: Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.

5 . Kuzimu humeza watenda maovu.

Ayubu 24:19 ----- Chaka na hari hukausha maji ya theluji. Kuzimu [sheol] wako ambao wamefanya dhambi.

6. Mauti na kuzimu (waendako wafu) ni vitu vilivyofungamana pamoja.

Zaburi 6:5 ----- Maana mauti hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu [waendako wafu] ni nani atakaye kushukuru?

7. Kuzimuni [Sheol], waendapo wafu, hakutakoma milele.

Zaburi 49:15 ----- Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu.

8. Kutakuwa na mwisho wa kuzimuni.

Hosea 13:14 ----- 0 grave,[sheol] I will be thy destruction.

(Kumbuka: Sheol ni neno lililotumika katika Agano la Kale ambalo limetafsiriwa na kuitwa kuzimu. Kuzimu ni lilimaanisha kuwa ni mahali pa wafu).

Hades, neno lingine la kuelezea kuzimuni katika Agano Jipya ni neno la Kiyunani lenye maana ile ile ya sheol, kama ilivyotafsiriwa kuwa kaburi na linaonekana mara 1 tu, na kuzimuni [hell] mara10. Lina maana ile ile kama ya mahali waendako wafu.

Mathayo 11:23 ----- Nawe Kapernaum, ... utashushwa mpaka kuzimu [hades].

Mathayo 16:18 ----- nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu [waendako wafu, kaburi] haitaweza kulishinda.

Luka 16:23 ----- Basi kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso.

Matendo 2:27 ----- hutaiacha roho yangu katika kuzimu.

Matendo 2:31 ----- kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu [hades].

1 Wakorintho 15:55 ----- Ku wapi, Ewe mauti kushinda kwako? [hades, pia]

Ufunuo wa Yohana 1: 18----- Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu [grave].

Ufunuo wa Yohana 6:8 ----- jina lake ni Mauti, na Kuzimu [hades, kaburi] akafuatana naye.

Ufunuo wa Yohana 20:13 ----- na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu sawa sawa na matendo yake. (Kumbuka: Hukumu yao ilifanyika baada ya kutoka kuzimuni [yaani kaburini]).

Ufunuo wa Yohana 20:14 ----- Mauti na Kuzimu zikatupwa kwenye lile ziwa la moto. (Kumbuka: Kuzimu moja itatupwa kwenye nyingine ina maana kwamba. Kuzimu ya "Hades" itatupwa kwenye ile kuu ya Jehanamu [Gehenna]. Ambayo ni Kuzimu ya ziwa la moto).

Ziwa la Moto Kuzimuni ----- Hatimaye

Jehanamu (Gehenna), ni neno la ki Agano Jipya, la Kiyunani, lenye maana ya kuzimu ya ziwa la moto, ambalo limetumika mara 12, likimaanisha pia kuwa ni ziwa la moto, litakalotumiwa na Mungu kuwaangamiza waovu baada ya kuhukumiwa kwao.

Mathayo 5:22 ----- imempasa jehanum ya moto.

Mathayo 5:29,30-----mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.

Mathayo 10:28 ----- kuangamiza mwili na roho pia kataka jehanum.

Mathayo 23:15 ----- mnawafanya wana wa jehanum [kuzimu motoni] mara mbili zaidi kuliko ninyi eenyewe.

Mathayo 23:33 ----- mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? [Gehenna, kuzimu-motoni].

Marko 9:43 ----- kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanuml.

Marko 9.45 ----- kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum.

Marko 9:47 ----- kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehnum ya moto. (Tazama pia, Isaya 66:24).

Luka 12:5 ----- akisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika jehanum.

Yakobo 3:6 ----- ulimi ... nao huwashwa moto wa jehanum. (Kumbuka: Ziwa la moto linaitwa mauti ya pili, (Ufunuo wa Yohana 20:14; 21:8). (Kumbuka pia kuhusu moto kwa kusoma Zaburi 21:9; 37:20; Malaki 4:1-3; Mathayo 3:12; 2 Wathesalonike 1:7- 10; 2 Petro 3:7, 10-12.)

MWOKOZI WA MWANADAMU, BWANA WETU YESU KRISTO

Yesu, Mwana wa Mungu

Mathayo 14:33 ----- Hakikawewe ni Mwana wa Mungu.

Mathayo 16:16 ----- Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.

Mathayo 27:54 ----- Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

Marko 3:11 ----- Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.

Luka 1:35 ----- Malaika ... akambambia ... hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu

Yohana 1:34 ----- Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.

Yohana 3:16 ----- Kwa maana jinsi hii Mungu ... akamtoa Mwanawe pekee.

Yohana 3:18 ----- Mwana pekee wa Mungu.

Yohana 5:25 ----- wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu.

Yohana 9:35, 36, 37 ----- Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?. . . Ni nani, Bwana? ... naye asemaye nawe ndiye.

Yohana 10:36 ----- yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?

Yohana 20:31 ----- Lakini hizi zimeandikwa; ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu.

Matendo 8:37 ----- Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.

Matendo 9:20 ----- Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.

Waebrania 4:14 ----- tunaye kuhani mkuu … Yesu Mwana wa Mungu.

Yesu -----Alitumwa Toka kwa Mungu Kuokoa Waliopotea

Mathayo 1:21----- maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

Marko 10:45 ----- Mwana wa Adamu naye hakuja … bali kutumika, na kuitoa nafsi yake kwa fidia ya wengi

Luka 19: 10 ----- Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea.

Wagalatia 4:4, 5 ----- Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa mwanamke … kusudi awakomboe.

Yesu -----Alitumwa Kumkomboa Mwanadamu Toka Dhambini

Warumi 3:24 ----- wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.

waefeso 1:7 ----- Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi.

Wakolosai 1: 14---- - ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, masamaha ya dhambi.

Tito 2:14 ----- ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na masi yote

1 Petro 1: 18, 19 ----- mlikombolewa ... kwa damu ya thamani, … ya Kristo.

Yesu Mwenyewe Hakuwa na Dhambi

Yohana 8:46 ----- Ni nani anishuhudiaye miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa ninadhambi?

2 Wakorintho 5:21 -----alimfanya [Yesu] kuwa dhambi kwa ajili yetu.

Waebrania 4:14, 15 ----- Yesu ... alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote katika mambo yote, bila kuganya dhambi.

1 Petro 2:22 ----- Yeye hakutenda dhambi.

1 Yohana 3:5 ----- yeye alidhihirishwa , ili aliondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.

Akiwa Hana Dhambi, Alifanyika Kuwa ni Dhabihu Kamilifu

1 Wakorintho 5:7 ----- Kwa maana Pasaka wetu amekwisha tolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.

Waebrania 9:26 ----- alidhihirishwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake

1 Petro 1:18, 19 ----- mlikombolewa ... kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.

Yesu Kristo ni Mwokozi Pekee

Yohana 14:6 ----- Yesu akamwambia ... Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Matendo 4:12 ----- Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Yesu Kristo Alikufa, Alizikwa, Akafufuka

1 Wakorintho 15:3 -----Kristo alikufa.

Warumi 14:9 ----- Kristo alikufa akawa hai.

2 Wakorintho 5:14 ----- mmoja alikufa kwa ajili ya wote.

Wagalatia 2:20 ----- Kristo ... alijitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

1 Wathesalonike 5:9, 10 ----- Bwana wetu Yesu Kristo … alikufa kwa ajili yetu.

Yohana 19:41, 42 ----- kaburi jipya ... wakamweka Yesu.

Marko 15:45, 46 ----- Yusufu ... akamteremsha, akamfunga ile sanda, akamweka katika kaburi.

Matendo 13:30 ----- Lakini Mungu akamfufua katika wafu.

Matendo 3:15 ----- mkamwua yule aliye Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu.

2 Wakorintho 4:14 ----- yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu.

Na Sasa Anatuombea Mbinguni

Warumi 8:34 ----- Kristo Yesu ... yuko mkono wa kuume wa Mungu .... ndiye anayetuombea.

1 Timotheo 2:5 ----- mpataishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu.

Waebrania 7:25 ----- yu hai sikuzote awaombee.

1 Yohana 2:1 ----- tunaye mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki.

Kristo Anakuja Tena ----- Mara ya Pili, Yeye Mwenyewe na Ataonekana, Kwa Nguvu na Utukufu

Ayubu 19:25 ----- Mtetezi wangu yu hai, Na . . . atasimama juu ya nchi.

Mathayo 24:27 ----- Kwa maana kama vile umeme … ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Mathayo 24:30----- watamuona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

Luka 18:8----- atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataone imani duniani?

Yohana 14:3 -----nitakuja tena niwakaribisha kwangu

Matendo 1:11 -----Huyo Yesu ... atakuja jinsi iyo hiyo mliyomwona akienda zake.

Matendo 3:20 ----- apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani.

1 Wakorintho 1:7 ----- mkitazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

1 Wakorintho 11:26 ----- Maana kila muulapo ... mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

1 Wakorintho 15:23 ----- limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.

Wafilipi 3:20 ----- mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo.

1 Wathesalonike 1:10 ----- na kumngoja Mwanawe kutoka mbinguni.

1 Wathesalonike 3:13 ----- wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.

1 Wathesalonke 4:15 ----- tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana.

1 Wathesalonke 4:16 ----- Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni.

2 Wathesalonike 1:7 ----- Bwana Yesu kutoka mbinguni.

2 Wathesalonike 1:10 ----- yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu.

2 Wathesalonike 3:5 ----- Bwana ... pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.

Tito 2:13 ----- mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu.

Waebrania 9:28 ----- atatokea mara ya pili.

1 Yohana 3:2 ----- atakapodhihirikawa, tutafanana naye … tutamuona.

Ufunuo wa Yohana 1:7 ----- Tazama, yuaja na mawingu, na kila jicho litamuona.

Mambo Haya Yamhusuyo Yesu Kristo Ni Miongoni Mwa Injili (Ionyeshayo Jinsi Dhambi Inavyoweza Kusamehewa)

1 Wakorintho 15:1-4 ----- Injili niliyowahubiri; ... ya kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, … alizikwa … alifufuka.

Matendo 8:5, 12----- Filipo ... akawahubiri Kristo ... walipomwamini Filipo, akihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo.

Matendo 28:23 ----- na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu.

Matendo 28:30, 31 ----- [Paulo] … akiwahubiri habari za Ufalme wa Mungu, na kuwafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo.

UFALME WA MILELE WA MUNGU

Sehemu Nyingine ya Injili Kuhusiana na Ufalme wa Mungu (Makao Yajayo ya Milele ya Waliokombolewa, Wokovu Wetu Utakapokamilika)

Mathayo 4:23 ----- Naye alikuwa akizunguka ... akifundisha ... katika masinagagi yao, na kufundisha Habari Njema ya ufalme, na kuponya.

Marko 1: 14 ----- Yesu akaenda ... akiihubiri Habari Njema ya Mungu.

Luka 4:43 -----imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa.

Luka 8:1 ----- alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kufundisha habari njema ya ufalme wa Mungu.

Matendo 1:3 ----- siku arobaini ... kuyanena mambo yahusuyo ufalme wa Mungu.

Matendo 8:12 ----- Filipo, akihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo.

Matendo 19:6, 8 -----Paulo ... akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.

Matendo 20:25 ----- ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu.

Matendo 28:23 ----- na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu.

Matendo 28:31 ----- akiwahubiri habari za Ufalme wa Mungu, na kuwafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo.

Ufalme wa Mungu Bado ni Kwa Siku za Zinazokuja Mbele

Danieli 2:44 ----- Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa … utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.

Danieli 7:27 ----- Na ufalme, ... chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; … na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.

Mathayo 6:33 ----- Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake.

Luka 19:11 -----aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara.

Matendo 1:6 ----- je! Bwana, wakati huu ndipo utakapowarudishia Israeli ,ufalme?

Luka 21:31----- Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.

Luka 23:51 ----- tena anautazamia ufalme wa Mungu.

Ufunuo wa Yohana 11:15----- Malaika wa saba akapiga baragumu ... Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.

Utakuwa Hapahapa Duniani

Zaburi 72:8 ----- Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka Mto hata miisho ya dunia.

Isaya 2:2, 3, 4 ----- na mataifa yote watauendea makundi makundi … na kusema, Njooni, twende juu mlimani mwa BWANA … maana katika Sayuni kutatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa yote.

Isaya 26:9 ----- Maana hukumu zako zikiwapo duniani, watu wakaao duniani hujifunza haki.

Isaya 42:4 ----- Hatazimia. . . atakapoweka hukumu duniani.

Isaya 45:18 ----- Yeye ni Mungu . . . ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya ... aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu.

Yeremia 23:5 ----- mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.

Yeremia 33: 15 ----- naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii.

Danieli 7:27 ----- Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu … na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.

Habakuki 2:14 ----- Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari.

Zekaria 9: 10 ----- na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya nchi.

Zekaria 14:17 ----- kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme.

Zekaria 8:22 ----- Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta BWANA wa majeshi.

Mathayo 24:30 ----- ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamuona Mwana wa Adamu akija.

Matendo 17:26 ----- Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wan chi yote.

Ufunuo wa Yohana 11:15----- Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.

Ufunuo wa Yohana 21:2 ----- Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.

Ufunuo wa Yohana 21:24 ----- Na mataifa watatembea katika nuru yake.

Nchi Itadumu na Kuwepo Milele

1 Nyakati 16:30 -----ulimwengu utathibitika usitikisike.

Zaburi 104:5 ----- Uliiweka [Mungu] nchi juu ya misingi yake, Isitikisike milele.

Zaburi 119:90 ----- uliiweka nchi nayo ikakaa.

Zaburi 148:6 ----- Amevithibitisha hata milele na milele, Ametoa amri wala haitapita.

Mhubiri 1:4 ----- nayo dunia hudumu milele.

Isaya 45:18 ----- Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ... aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu.

Nchi Itakombolewa Kutokakana na Laana, Kufanywa Upya na Kutukuka

Hesabu 14:21 ----- lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA.

Zaburi 102:25, 26 ----- nchi, Na mbingu … zitabadilika.

Waebrania 1: 12 ----- Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika.

Isaya 65:17 ----- Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya; na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.

Isaya 66:22 ----- Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya.

2 Petro 3:13 ----- Lakini kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya ambayo haki yakaa ndani yake.

Ufunuo wa Yohana 21:1 ----- Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya.

Ufunuo wa Yohana 21:4 ----- Naye afuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Ufunuo wa Yohana 21:5 ----- Tazama, nayafanya yote kuwa mapya (haisemi kuwa, nafanya vitu vyote viwe vipya].

Isaya 11:9 ----- dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari.

Habakuki 2:14 ----- Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari.

Mathayo 6:10 ----- Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama mbinguni.

Matendo 3:19 ----- nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.

Matendo 3:21 ----- zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizinenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.

Warumi 8:22, 23 ----- viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. Wala si hivyo tu; na sisi wenyewe … pia tunaugua … tukitazamia kufanywa wana..

Ufunuo wa Yohana 22:3 -----Wala hapatakuwa na laana tena.

Nchi, Urithi wa Milele wa Watakatifu

Mathayo 5:5----- wenye upole ... watairithi nchi.

Zaburi 25:13 ----- Wazao wake watairithi nchi.

Zaburi 37:9 ----- Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.

Zaburi 37:11----- Bali wenye upole watairiti nchi.

Zaburi 37:18 ----- Na urithi wao utakuwa wa milele.

Zaburi 37:22---- - Maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi.

Zaburi 37:29 ----- Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.

Zaburi 37:34 ----- Naye atakutukuza uirithi nchi, Wasio haki watakapoharibiwa utawaona.

Zaburi 115:16 ----- Mbingu ni mbingu za BWANA, bali nchi amewapa wanadamu.

Mithali 10:30 ----- Mwenye haki hataondolewa milele, Bali wasio haki hawatakaa katika nchi milele.

Mithali 11:31 ----- Tazama, mwenye haki atalipwa duniani.

Isaya 45:18 ----- hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu.

Danieli 7:27 ----- ufalme, chini ya mbingu … na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.

Mathayo 6:10 ----- Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama mbinguni.

Ufunuo wa Yohana 5:10 -----nao watamiliki juu ya nchi.

Ufunuo wa Yohana 11:15 ----- Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake … atamiliki hata milele na milele.

Urithi wa Nchi Uliahidiwa Kupitia Agano la Ibrahimu

Mwanzo 13:14, 15 ----- inua sasa macho yako, ... upanse wa kaskazini, na upande wa kusini, na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.

Mwanzo 17:7, 8----- Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako … kuwa agano la milele. Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii … nchi yote ya Kanaani kuwa milki yako.

Mwanzo 22:17, 18 ----- na uzao wako watamiliki malango ya adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa.

Matendo 7:5 ----- Wala [Mungu] hakumpa [Ibrahamu] urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi … uzao wake.

Warumi 4:13 ----- ahadi ... mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa kwa imani.

Warumi 4:16----- ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; … si … wale wa torati … na kwa wale walio wa imani ya Ibrihimu; aliye baba yetu sisi sote.

Warumi 15:8 ----- Kristo alifanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu.

Wagalatia 3:16 ----- Basi ahadi imenenwa kwa Ibrahimu na Kwa Mzao wake [Kristo].

Wagalatia 3:18 ----- uruthi ... kwa ahadi.

Wagalatia 3:29 ----- Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawa sawa na ahadi.

Wagalatia 4:28 ----- Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.

Waebrania 11:8 ----- Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi akatoka asijue aendako.

Waebrania 11:9 ----- ugenini katika ile nchi ya ahadi.

Waebrania 11:13 ----- Hawa yote walikufa katika imani, wasijazipokea zile ahadi. [Ahadi ile itakuja kutimia. Kama tunavyosoma jinsi Yesu alivyosema]:-

Luka 13:28, 29 ----- [Aliwaambia Wayahudi watendadhambi]: mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, wenyewe mmetupwa nje. Nao watakuja watu toka mashariki … magharibi … kaskazini … kusini … nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu

Kristo Atatawala Akiwa ni Mfalme wa Dunia Hii Kwa Kipindi Cha Miaka Elfu, na Atawaseta Maadui Zake Chini ya Miguu Yake

Ufunuo wa Yohana 20:4 ----- watatawala pamoja na Kristo miaka elfu.

Ufunuo wa Yohana 20:6 ----- watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.

Zaburi 2:6 ----- Nami nitaweka mfalme wangu Juu ya Sayuni mji wangu mtakatifu.

Zaburi 2:8 ----- Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.

Zaburi 2:9 -----Utawaponda kwa fimbo ya chuma.

Zaburi 72:9 ----- Adui zake na warambe mavumbi.

Zaburi 72:11 -----Naam, wafalme wotena wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.

Zaburi 110:1 ----- Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Ukti mono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo maadui zako Kuwa chini ya miguu yako.

Zaburi 110:2 ----- BWANA atanyoosha toka Sayuni Fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako.

Isaya 2:4 ----- Naye atafanya hukumu katika mataifa mengiatawakemea watu wa kabila nyingi.

Isaya 9:6 ----- uweza wa kifale utakuwa begani mwake.

Isaya 9:7 ----- Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele.

Yeremia 23:5 ----- mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.

Yeremia 33:15 ----- chipukizi la haki; naye atafanya hukumu ya haki katika nchi hii.

Mathayo 13:41 ----- Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maovu.

Mathayo 19:28 ----- katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake.

Mathayo 25:31 ----- Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake … ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake.

Luka 1:32 ----- Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

Luka 1:33 -----Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele … ufalme wake hautakuwa na mwisho.

Luka 22:29 ----- Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi.

Luka 22:30 ----- mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika kiti cha enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

Matendo 2:30 ----- Mungu alimwapia kwa kiapo … atamketisha mmoja [Kristo] katika kiti chake cha enzi [Daudi].

1 Wakorintho 15:24 ----- atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

1 Wakorintho 15:25 ----- Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.

1 Wakorintho 15:28 ----- Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake.

Waebrania 10:13 ----- tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake.

Ufunuo wa Yohana 1: 5 ----- Yesu Kristo … mkuu wa wafalme wa dunia.

Ufunuo wa Yohana 11:15 ----- Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake.

Ufunuo wa Yohana 12:5 ----- yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma.

Ufunuo wa Yohana 19:15 ----- Naye atawachunga [mataifa] kwa fimbo ya chuma.

Ufunuo wa Yohana 19:16 ----- MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Jambo Hili Litatilimiliza Agano la Daudi

2 Samweli 7:12 ----- nitainua mzao wako nyuma yako, … nitaufanya imara ufaIme wake.

2 Samweli 7:13 ----- kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara miIele.

2 Samweli 7:16 ----- Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako, Nacho kiti chako kitafanywa imara milele.

1 Nyakati 17:14 ----- na kiti chake cha enzi kitathibitika milele.

1 Nyakati 28:5 ----- Sulemani … aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli.

1 Nyakati 29:23 ----- Ndipo Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha BWANA, awe mfalme badala ya Daudi babaye.

Yeremia 33:17 ----- Daud hatakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli.

Yeremia 33:20,21 ----- Kama mkiweza kulivunja agano Iangu la mchana, na … la usiku, … ndipo agano langu nililolifanya na Daudi … hata asiwe na mwana wa kumiliki katika kiti chake cha enzi.

Ezekieli 21:26, 27 ----- Kiondoe kilemba, ivue taji … Nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa.

Luka 1:32 ----- na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

Matendo 2:30 ----- katika uzao wa viuno vuake atamketisha mmoja [Kristo] katika kiti chake cha enzi.

Mathayo 25:31 ----- Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake … ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake.

Watakatifu Wake Kristo Watatawala Pamoja Naye

Ufunuo wa Yohana 20:4 ----- nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.

Ufunuo wa Yohana 20:6 ----- watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.

Mathayo 25:21, 23 ----- mwaminifu ... nitakuweka juu ya mengi: ingia.

Luka 12:44 ----- atamweka juu ya vitu vyake vyote.

Luka 19:17 ----- uwe na mamlaka juu ya miji kumi.

Luka 19:19 ----- Wewe uwe juu ya miji mitatu.

Warumi 8:17 ----- warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo.

1 Wakorintho 4:8 -----Iaiti.. . ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi!

2 Timotheo 2:12 ----- Kama tukistahimili, tutamiIiki pamoja naye.

Ufunuo wa Yohana 3:21 ----- Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi.

Ufunuo wa Yohana 5: I0 ----- kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao watamiliki juu ya nchi.

Ufunuo wa Yohana 22:5 ----- watatawala hata milele na milele.

Taifa la Israeli Litapewa Milki Yake

Mwanzo 15:18 ----- Uzao wako nimewapo nchi hii.

Mwanzo 17:7, 8 ----- agano la milele ... Nami nitakupa wewe na uzao wako … nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya mileIe.

Isaya 11:11, 12 ----- BWANA atapeleka … mara ya pili … awape watu wake waliosalia … atawakutanisha watu wa Israeli … watu wa Yuda waliotawanyika.

Yeremia 30:10 ----- Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe.

Yeremia 23:6 ----- Katika siku zake Yuda atakombolewa, na Israeli atakaa salama.

Yeremia 31:31 -----nitakapofanya agano jipya na … Israeli, na … Yuda.

Yeremia 33:16 ----- Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu watakaa salama.

Ezekieli 36:33 -----nitaifanya miji ikaliwa na watu.

Ezekieli 36:35 ----- Nchi hiii, iliyokuwa ukiwa, imekuwa kama bustani ya Edeni.

Ezekieli 37:22 ----- nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo .. wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena.

Ezekieli 37:25 ----- Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo.

Ezekieli 47:13 ----- mtaigawanya nchi iwe urithi.

Ezekieli 47:14 ----- nchi hii itawaangukia kuwa urithi.

Ezekieli 47:21 ----- mtakavyojigawanyia … nchi hii … kabila za isreeli.

Ezekieli 48:29 ----- Hiyo ndiyo nchi mtakazozigawanyia.

Luka 1:33 ----- Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele.

Warumi 11:26 ----- Hivyo Israeli wote wataokolewa.

Mitume Kumi na Mbili Watazihukumu Kabila Kumi na Mbili ya Israeli

Mathayo 19:28 ----- ninyi ... mtaketi katika viti kumi na viwili, mtawahukumu kabila kumi na mbili za lsraeli

Luka 22:29, 30 ----- nanyi ndinyi ... na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahumuku kabila kumi na mbili za Israeli..

Makao Makuu ya Ulimwengu ----- Yerusalemu

Isaya 2:3 ----- katika Sayuni kutatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu.

Isaya 24:23 ----- kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu.

Isaya 62:7 ----- mpaka atakapoifanya imara Yerusalemu … kuifanya kuwa sifa duniani.

Isaya 65:18 ----- naumba Yerusalemu uwe shangwe.

Yoeli 3:17 ----- BWANA, Mungu wenu, akaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu … wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.

Zekaria 2:12 ----- BWANA ... atachagua Yerusalem tena.

Zekaria 8:3 ----- Mimi nimerudi... nitakaa ... Yerusalemu ... Mji wa kweli ... Mlima mtakatifu.

Zekaria 8:22 ----- watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta BWANA … na kuomba fadhili za BWANA.

Zekaria 14:16, 17 ----- kupigana na Yerusalemu kumwabudu Mfalme, BWANA.

Mathayo 5:35 ----- Yerusalemu ... mji wa Ufalme mkuu.

Waebrania 11:10----- Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.

Waebrania 12:22 ----- Bali ninyi mmeufikilia Mlima Sayuni, mji wa Mungu aliye hai.

Ufunuo wa Yohana 3:12 ----- mji wa Mungu ... Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni.

Ufunuo wa Yohana 21:2 ----- Nami [Yohana] nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni.

Ufunuo wa Yohana 21:3 ----- maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani pamoja nao, … Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Ufunuo wa Yohana 21:I0 ----- Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu.

Ufunuo wa Yohana 21:22 ----- sikuona hekalu ... Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana Kondoo, ndio hekalu lao.

Mataifa Watakaokuwepo (Kipindi Hiki Cha Miaka Elfu) Watajifunza Njia za Mungu

Zaburi 72:11 ----- mataifa yote watamtumikia.

Isaya 2:3 ----- atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake.

Isaya 2:4 ----- watafuta panga zao ziwe majembe … taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.

Isaya 11:9 ----- Hawatadhuru wala hawataharibu … mlima wangu wote mtakatifu … dunia itajawa na kumjua BWANA.

Isaya 11:10 ----- shina la Yese ... ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta.

Isaya 11:12 ----- Naye atawatwekea mataifa bendera.

Isaya 60:12 ----- Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu Wasiotaka kukutumikia wataangamia.

Yeremia 3:17 ----- Wakati ule ... Yerusalemu kiti cha enzi cha BWANA; na mataifa yote watakusanyika huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la BWANA.

Danieli 7:14 ----- watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote wamtumikie.

Danieli 7:27 ----- na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.

Zekaria 8:21 ----- Haya! Twendeni zetu … tukaombe fadhili za BWANA.

Zekaria 8:22 ----- Naam, watu wa kabila nyingi … watakuja Yerusalemu kumtafuta BWANA.

Mathayo 25:32 ----- na mataifa yote watakusanyika mbele zake … atawabagua.

Ufunuo wa Yohana 22:2 ----- mti wa uzima ... na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

Ezekieli 47:12 ----- matunda … chakula … majani … dawa.

Ufunuo wa Yohana 21:24 ----- mataifa watatembea katika nuru yake.

Adui wa Mwisho ----- Mauti ----- Ataharibiwa

1 Wakorintho 15:26 ----- Adui wa mwisho atakaye batilishwa ni mauti.

Ufunuo wa Yohana 20:14 ----- Mauti na kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto.

Ufunuo wa Yohana 21:4 ----- wala mauti haitakuwapo tena.

Ufunuo wa Yohana 22:3 ----- Wala hapatakuwa na laana yo yote tena.

Kristo Atakabidhi Ufalme Mkamilifu kwa Baba Yake, Ili Mungu Awe Yote Katika Yote

1 Wakorintho 15:24 ----- mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake.

1 Wakorintho 15:28 -----Mwana … atatiishwa … kwamba Mungu awe yote katika wote.

Tito 2:13 ----- mafunuo ya utukufu … Mungu mkuu.

Ufunuo wa Yohana 21:3 ----- Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Ezekieli 37:28 ----- patakatifu pangu patakapokuwa katikati yao milele.

Ufunuo wa Yohana 22:3 ----- kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo.

Zekaria 14:9 ----- BWANA atakuwa Mfalme juu ya nchi.

Ishara Zinazoashiria Kuwa Kurudi Kwa Kristo Kupo Karibu

Mathayo 24:3 ----- ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?

Mathayo 16:3 ----- je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?

Danieli 12:4 ----- wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.

Mathayo 24:12 ----- kuomgezeka maasi.

2 Timotheo 3:13 ----- Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataongezaka, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.

2 Timotheo 3:1-5 ----- siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.

Luka 17:26 - 30 ----- Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu … kama ilivyokuwa siku za Lutu, … ndivyo itakavyokuwa siku ile atakavyofunuliwa Mwana wa Adamu.

Luka 21:11 a ----- kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi … njaa, na tauni.

Luka 21:11 b ----- na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.

1 Wathesalonike 5:3---- - Wakati wasemapo, Kuna amani na usalama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula.

Mathayo 24:14 ----- Tena habari njema … itahubiriwa katika ulimwengu wote, … hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

Walimu wa Uwongo

Mathayo 24:11 -----Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kuwadanganya wengi.

Mathayo 24:24 ----- Kwa maana watatokea Makristo wa uwongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapte kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

Marko 13:22 ----- kwa maana wataondokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, … hata hao wateule.

Luka 17:23 ----- Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo.

Mathayo 24:26 ----- msitoke, yumo uvunguni, msisadiki.

2 Wathesalonike 2:3 ----- akafunuliwa yule mtu wa kuasi.

2 Wathesalonike 2:9 ----- kuja kwake ni … Shetani, kwa uwezo … na ishara na ajabu za uongo.

2 Petro 2:1 ----- kwenu … kutakavyokuwa waalimu wa uongo.

Ukengeufu

Mathayo 24:12 ----- upendo wa wengi utapoa.

Luka 18:8 ----- je! akaiona imani duniani?

2 Wathesalonike 2:3 ----- kwanza ule ukengeufu.

1 Timotheo 4:1 ----- wengine watajitenga na imani.

2 Petro 2:2----- Na wengi watafuata ufisadi wao.

Ishara za Mbinguni

Isaya 13:10 -----nyota … havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza … mwezi utaacha nuru yake kuangaza.

Isaya 13:13 ----- Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu.

Ezekieli 32:7 ----- nyota … kuwa giza … nitafunika jua … mwezi hautatoa nuru.

Yoeli 2:31 ----- Jua litageuzwa kuwa giza, … mwezi kuwa damu.

Yoeli 3:15 ----- Juan a mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza.

Hagai 2:6 -----nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu.

Ishara za Duniani

Luka 21:25 ----- ishara ... katika nchi dhiki ya mataifa.

Luka 21:26 ----- watu wakivunjika mioyo.

Marko 13:19 ----- Kwa maana siku hizo kutakuwa na dhiki.

Mathayo 24:22 ----- Na kama siku hizo zisngalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote.

Ufunuo wa Yohana 16:18 ----- tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu mwanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa t etemeko hilo.

Ufunuo wa Yohana 16:20 ----- Kila kisiwa kikakimbia, na milima haikuonekana.

Ezekieli 38:20 ----- na kila ukuta ukaanguka chini.

Kurudi Kwa Waisraeli Kwenye Ardhi ya Palestina

Isaya 11:10 - 16 ----- Bwana atapeleka mono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia.

Isaya 14:1, 3 ----- Maana BWANA atamhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena, naye atawaweka katika nchi yao wenyewe.

Isaya 27:12, 13 ----- nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.

Isaya 43:1-7 -----nitaIeta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi; nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusini, Usizuie, waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.

Yeremia 16:14, 15 ----- ambapo hamtasema tena, Aishivyo BWANA, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya Misri; Lakini, Aishivyo BWANA, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya kaskazini na toka nchi zote alizowafukuza; nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe niliyowapa baba zao.

Yeremia 24:5 - 7 ----- nitawaoa katika mahali hapa … nao watakuwa watu wangu.

Yeremia sura yote ya 30 inabeba ujumbe huu ----- nami nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, hao waimiliki.

Yeremia sura ya 31 inasema ----- Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

Yeremia 32:37 ----- Tazama, nitawakusanya, na kuwatoa katika nchi zote nilizowafukuza katika hasira yangu … nami nitawaleta tena hata mahali hapa, nami nitawakalisha salama salimini.

Ezekieli 36:24 ----- Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe

Amosi 9:11-15 ----- Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka … nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale; wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote … asema BWANA, afanyaye hayo.

Israeli, Kuwa Taifa Tena Katika Ardhi ya Palestina, Kuchangamanywa

Yoeli 3:2 ----- nitayakusanya mataifa yote … urithi … kuigawanya nchi yangu [Hii ilifanywa na Umoja wa Mataifa, Mwezi Mei 1948].

Ezekieli 38:8 ----- nitakukusanya toka kabila nyingi za watu.

Ezekieli 38:12 ----- ili kuteka mateka … juu ya watu waliokusanyika toka mataifa.

Ezekieli 38:16 ----- uwajilie watu wangu Israeli … itakuwa katika siku za mwisho.

Ezekieli 38:18 ----- siku hiyo, Gogu atakapokuja kupigana na nchi ya lsraeli ... ghadhabu yangu.

Zekaria 14:2 ----- nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu ... nao mji utapigwa.

Zekaria 14:1 ----- mateka watagawanyika

Luka 21:20 ----- Lakini hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi … uharibifu wake umekaribia.

Luka 21:31 ----- mwonapo mambo haya yanaanza kutokea … ufalme wa Mungu u karibu.

Watu wa Nyumbani Mwake Mungu

Mungu alimuita atoke mtu Aliyefanya kuwa ni mwaminifu kuliko watu wote waliowahi kuishi kwa nyakati zote.

Waefeso 2:19 - 22 ----- ninyi ... wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu ... mmejengwa juu ya mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jingo lote limeungamanishwa … hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.

Waefeso 3:6 ----- ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja na wa mwili mmoja.

Waefeso 4:4 ----- Mwili mmoja.

Matendo 7:38 ----- Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani.

1 Nyakati 28:8 ----- Israeli wote, hilo kusanyiko la BWANA.

Zaburi 149 ----- Watakatifu wake wote.

Luka 2:32 ----- Nuru ya kuwa mwangaza kwa Mataifa.

Yohana 10:16 ----- Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili.

Matendo 2:39 ----- Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote wataoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

Warumi 14:9 ----- Maana Krsto alikufa akawa hai kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai.

1 Wakorintho I0:1 - 5 ----- na Mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

Waebrania 11:40 ----- ili wasikamilishwe pasipo sisi.

Jina la Kanisa la Kweli

Tangu siku ya Pentekoste, kila mtu anayetamani kuwa ni mshiriki wa wale walio Nyumbani mwa Mungu, analazimika kuwa ni mshiriki wa mwili wa Kristo, ambao ni "kanisa". Bwana huwaongeza kwenye kanisa la kweli wale wanaostahili kwa njia ya imani na utii. Ni kanisa la Mungu, na amemuweka Mwanae Yesu Kristo kuwa ni Kichwa cha kanisa hili.

1 Petro 3:18 ----- Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi … ili atulete kwa Mungu.

Matendo 20:28 ----- mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

1 Wakorintho 1:1, 2 ----- Paulo ... na kwa kanisa la Mungu lililoko Koritho.

1 Wakorintho 10:32 ----- Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu.

1 Wakorintho 11:16 ----- Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala kanisa la Mungu.

1 Wakorintho 11:22 -----Je! Hamna nyumba ya kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu?

1 Wakorintho 15:9 ----- naliliudhi kanisa Ia Mungu.

2 Wakorintho 1:1 ----- Paulo ... kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho.

Wagalatia 1:13 ----- naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu.

1 Wathesalonike 2:14 ----- Maana ninyi ... mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu.

2 Wathesalonike 1:4 ----- sisi wenyewe twaona fahari juu yenu katika makanis ya Mungu kwa ajili ya saburi yenu.

1 Timotheo 3:5 ----- yaani mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalisimamiaje kanisa la Mungu?

1 Timotheo 3:15 ----- lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo ya msingi wa kweli.

Yohana 17:11 ----- Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa.

Matendo I5:14 ----- Mungu hapo kwanza aliwaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.

Waefeso 3:14, 15 ---- nampigia Baba magoti [Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo] ambaye kwa jina lake ubaba twote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

TUNAPASWA KUFANYA NINI KWA WOKOVU "MKUU"

Kuwa na Imani, Kuamini

Marko 1:15 ----- kuiamini injili

Marko 16:15,16 ----- mkaihubri injili … Aaminiye na kubatizwa ataokoka.

Matendo 8:12 -----Lakini walipomwamini … ufalme wa Mungu … jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.

Matendo 10:43 ----- kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.

Matendo 16:30, 31 ----- yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka.

Warumi 1:16 ----- Injili ... kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye.

Warumi 10: 17 ----- imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Waebrania 11:6 ----- Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, nwa kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Tubu

Marko 6:12 ----- wakahuri kwamba watu watubu.

Luka 13:3 ----- lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

Luka 24:47 ----- watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi.

Matendo 2:38 ----- Tubuni, mkabatizwe.

Matendo 3:19 ----- Tubuni basi, mrejee.

Matendo 11:18 ----- Basi Mungu akawajalia hata mataifa nao toba iletayo uzima.

Matendo 17:30 ----- Mungu … bali sasa amewaagiza watu wote wa kila mahali watubu.

Warumi 2:4 ----- wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?

2 Wakorintho 7: 10 ----- Maana huzuni iliyo kwa ajili ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu.

Ubatizwe

Marko 16:16 ----- Aaminiye [injili] na kubatizwa ataokoka.

Mathayo 28:19 ----- mkawafanye mataifa wote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza.

Matendo 2:38 ----- Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu.

Matendo 2:41 ----- nao waliolipokea neno lake wakabatizwa.

Matendo 8:12 ----- Lakini walipomwamini … ufalme wa Mungu … jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa.

Matendo 8:16 ----- wakabatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.

Matendo 8:36 ----- Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?

Matendo 8:37 ----- Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana.

Matendo 8:38 ----- wakatelemka wote wawili majini … naye akambatiza.

Matendo 16: 15 ----- alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake.

Matendo 16:33 -----kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote.

Matendo 18:8 ----- Na Krispo ... pamoja na nyumba yake yote; Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa.

Matendo 9:18 ----- akasimama [Paulo] akabatizwa.

Mathayo 3:16 ----- Naye Yesu ... alipokwisha kubatizwa.

Warumi 6:3 ----- sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tilibatizwa katika mauti yake?

Warumi 6:4 ----- tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake … tuenende katika upya wa uzima.

1 Wakorintho 12:13 ----- Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja.

Wagalatia 3:27 ----- Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

Wakolosai 2:12 ----- Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo.

Ishi Maisha Matakatifu – Ikulie Neema na Kumjua Kristo

Waebrania 6:1 ----- tuukaze mwendo tuufikilie ukamilifu.

Mathayo 10:22 ----- mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka.

2 Petro 1:5 - 11 ----- kwa upande wenu katika imani … maarifa … kiasi … saburi … utauwa … upendano wa ndugu … upendo.

2 Petro 1:10 ----- kufanya imara kuitwa kwenu … mkitenda hayo hamtajikwa kamwe.

Wagalatia 5:22, 23 ----- Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.

Mathayo 22:37, 39 ----- Mpande Bwana, Mungu wako kwa moyo wako wote ... Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Luka 6:31 ----- Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendei vivyo hivyo.

Warumi 6:22 ----- Lakini sasa ... na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu ndiyo kutakaswa.

Warumi 12:9 ----- lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.

Warumi 12:12 ----- kwa tumaini, mkifurahi; kwa dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu.

Warumi 12:21 ----- Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Wagalatia 2:20 ----- Kristo yu hai ndani yangu.

Wagalatia 6:1 ----- Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole.

Wagalatia 6:2 ----- Mchukuliane mizigo.

Waefeso 4:32 ----- tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane.

Wafilipi 4:13 -----Nayaweza mambo yote kwake yeye anitiaye nguvu.

I Wakorintho 10:13 ----- Mungu … hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini … atafanya mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

2 Timotheo 3:16, 17 ----- Kila andiko … lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

Waebrania 4:16 ----- tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kuwasaida wakati wa mahitaji.

Yakobo 5:16 ----- na kuombeana … Kuomba kwake mwenye haki kwa faa sana akiomba kwa bidii.

1 Petro 2:21 ----- Kristo ... kielelezo, mfuate nyayo zake.

1 Petro 3:12 ----- macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maobi yao.

1 Petro 3:15 ----- Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu … habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.

1 Petro 5:6 ----- nyenyekeeni chini ya mkono wa Bwana ulio hodari.

Mathayo 7:20 ----- Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.

Mathayo 11:28 ----- Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Ndipo tunaweza kusema kama alivyosema Paulo:

2 Timotheo 4:7, 8 -----Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda. Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu wenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake..

Jarida hili haliruhusiwi kufanyiwa mabadiliko au kuhaririwa kwa namna yo yote iile.

REJEA KWENYE UKURASA MKUU