KALENDA YA PASAKA
Tarehe 19, Aprili, 2008, tangia Saa 12:00 Jioni—Apeili 20, 2008 Saa 12:00 Jioni.
Na James Herschel Lyda
Katika siku zetu hizi za leo, tunaweka siku, majuma, miezi na miaka kwa tukituama kwenye utaratibu wa kalenda iliyotungwa na kuanzishwa na Papa wa Kirumi Gregory XIII na kutangazwa rasmi itumike mnamo tarehe24, Februari 1582. Kalenda hii ambayo inajulikana pia kama Kalenda ya Gregory, ndiyo kalenda pekee iliyoenea zaidi ulimwenguni na kutumiwa na watu wengi hapa Duniani. Kalenda hii ya Kigregoriani ambayo mpangilio wake unategemea mzunguko wa jua, ni kalenda liyotuama kwenye muundo wa kisayansi wa kimahesabu. Inahesabia siku kuwa ni kigezo muhimu cha wasaa, ikiweka majumlisho ya mwaka wenye jumla ya siku 365 au 366 ambayo siku zake huhesabiwa kuanzia saa 6:00 ya usiku wa manane na kuishia usiku wa manane wa siku inayofuatia.
Je, ni kwa nini basi sisi tujumuike kwenye matendo haya ya kipagani na kuacha kuhimidi yale ambayo Mungu wetu Wapekee na wa Kweli aliyaweka na kutuagiza? Alisema hivi:
Kutoka 12: 1 BWANA akanena na Musa, na Haruni katika nchi ya Misri akawaambia,
2
Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.Kumbukumbu La Torati 16:1Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA, Mungu wako.
Mwezi.
Tangu wakati wa kuanzishwa kwa Sheria za Musa, utaratibu wa kuhesa miezi uliojulikana kwa Wayahudi ulikuwa ni ule wa Miandanmo ya Mwezi lakini ilihusiana na mwelekeo wa machweo ya jua. Utaratibu wa mzunguko hadi kufikia siku za maadhimisho ya sikukuu za kidini ilitegemea sana na miandamo ya mwezi. Mwaka wa kidini ulianza katika kipindi kinachokaribiana na kile cha uski na mchana huwa na muda sawa katika mzunguko wa jua linapopita katikati ya mstari wa Ikweta (mwanzoni mwa majira ya baridi), yapata kama tarehe 21 Marchi. Utaratibu wa kuhesabu mwanzo wa mwezi ulianzia na mwandamo wa mwezi mpya. Kwa maneno mengine ni kwamba ulianzia katika maadhimiso ya mwandamo wa mwezi mpya kwa maneno mengine ni kwamba, mwaka ulianzia katika muandamo wa mwezi mpya uliofuatia mwanzo wa majira ya baridi. Kuna mambo yakupendeza kuyajua kuhusiana na hali hii. Inaonekana kwamba dunia iliumbwa katika kipindi hiki cha majira ya baridi wakti wa kipindi kile cha Uumbaji. Pia baada ya gharika kuu, Nuhu alifungua mlango wa Safina na kutoka kuanza maisha mapya kwenye Ulimwengu Mpya katika kipindi hiki cha baridi cha mwaka ule. Wana wa Israeli pia walitoka kutoka nchi ya utumwa ya Misri katika kipindi hiki hiki cha majira ya baridi. Kipindi hiki cha majira ya baridi ni cha kufanywa tena kwa mambo yote katika asili zake, ni ishara ya uumbaji mpya wa Mungu wa maisha mapya. Mwezi huu wa Abibu hatimaye ulijulikana kama mwezi wa Nisani.
Usiku wa Pasaka ulitolewa kwa Waisraeli miaka mingi sana kabla ya Kristo, lakini ilionyehsa kikamilifu usahihi wa mwezi na siku ambayo Kristo alipaswa kufa msalabani. Ilionyosha kwamba yeye alipaswa kuwa ndiye Mwana Kondoo wa Mungu asiye na dhambi wala waa lolote. Hii ni moja kati ya sikukuu ambazo tumeamriwa kuzitunza na kuziadhimisha milele. Siku nyingine muhimu zimeorodheshwa kawnye vitabu vifuatavyo:
Kutika 20: 8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Lakini Sabato ni lini? Sio Jumamosi kama wengine wanavyodhania. Pia sio Jumapili kama wengine wanavyoadhimisha. Lakini katika mwaka huu imetokea tu kwamba inaangukia siku ya Jumapili kuanzia saa 12:00 jioni hadi Jumatatu saa 12:00 jioni. Kwa mujibu wa mpango wa Mungu, mwezi wa kwanza unaanzia katika mwezi wa Abibu. Mwezi huu wa Abibu unaandama kwenye kipindi kilicho karibu na siku ambayo jua linapita katikati ya dunia kwenye mstari wa Ikweta, siku inayolingana masaa ya usiku na mchana (mwanzoni mwa majira ya baridi). Kwa mujibu wa utaratibu wa Mungu, mwaka mpya huanza tarehe 18 Marchi, saa 12:00 jioni na siku itaishia tarehe 19 Marchi, saa 12:00 jioni
Mwanzo 1:5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili
Hii ndiyo sababu kwamba siku inahesabiwa kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 12:00 ya jioni inayofuatia. Saa 12:00 jionii hadi 12:00 asubuhi ni masaa ya usiku na saa 12:00 asubuhi hadi 12:00 mchana ni masaa ya mchana.
Siku saba zinazofuatia tarehe 19 Marchi ambayo ni tarehe 24 Marchi, saa 12:00 jioni inakuwa ni siku ya saba maadhimisho ya Sabato. Imetokea tu mwaka huu siku hii kuwa ni Jumapili Usiku na Jumatatu Mchana. Mabadiliko kati ya mwaka mmoja hadi mwingine hutokea kwa kuwa kalenda yetu haizingatii ishara za mwandamo wa Mwezi.
Mwanzo 1:14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;
Lakini kalenda yetu mara nyingi huzingatia mwongozo wa jua ambalo wapagani huliabudu. Kwa mujibu wa matumizi ya kalenda tuliyonayo sasa ulimwenguni kote na ratiba za maisha yetu vinavyohusiana, inakonekana kuwa ni kama vigumu kuishi kwa kuitegemea kalenda hii Takatifu ya Mungu. Lakini siku moja inakuja ambayo kutatangazwa rasmi kuwa haya masaa hayana maana tena.
Warumi 14:5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa ni sawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.
6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Je, Usiku wa Kwanza wa Pasaka Utakuwa Lini? |
Usiku wa Kwanza wa Pasaka Katika Miaka ya 2006-2016. |
|
Aprili 12, 2006* |
|
Aprili 02, 2007* |
|
Aprili 19, 2008* |
|
Aprili 08, 2009* |
|
Marchi 29, 2010* |
|
Aprili 18, 2011* |
|
Aprili 06, 2012* |
|
Marchi 25, 2013* |
|
Aprili 14, 2014* |
|
Aprili 03, 2015* |
|
Aprili 22, 2016* |
|
*Siku Takatifu Zinaanza wakati Jua Linapozama |