JE, MWANADAMU ANA MAJUKUMU GANI?
Watati Mungu alipomuumba Mwanadamu alimpa uhuru wa kufanya maamuzi kati ya kumtumikia yeye (Mungu) au kumtumikia Shetani. Uamuzi wa kuchagua kati ya uzima na mauti.
- Luka 16:13 Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Huwezi kuwatumikia Mungu na mali.
- Kumbukumbu la Torati 30:19 Nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
- Kumbu kumbu la Torati 11:27 Baraka ni hapo mtakapoyasikia maneno ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo; 28 Na laana ni hapo msipoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, msikengeuke katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
Iwapo kama mwanadamu itachagua kumtumikia Mungu aliye hai wa pekee na wa kweli, basi atapata baraka nyingi zisizoweza kufananishwa, lakini kama utaamua kutumikia uovu basi kutakuwa na laana ya mwisho ya mauti ambayo haina kurudi tena.
Basi ni wajibu wa mwanadamu kumchagua Mungu huyu wa pekee na wa kweli, Yehova, na kuzishika amri na sheria zake zote.
- Mhubiri 12: 13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndivyo impasavyo mtu.
- Mathayo 5: 48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Basi, ni juu yetu kuamua kuchagua kumfuata Yehova kwa kujitahidi kuwa wakamilifu katika utumshi wetu kwake. Tunapaswa kujitahidi kuzifuata amri na njia zake zote kwa siku zetu zote zilizobakia za maisha yetu.
- Zaburi 119:4 Wewe umeuamuru musia yako, Ili sisi tuyatii sana. Yohana 15:10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
Ni kazi yetu pia kuishi maisha yetu kwa njia kama hii ambayo kwayo tutafanyika kuwa ni mfano mzuri kwa wengine. Tunapaswa kila wakati kuwa tayari kuwa na jibu la kwa nini, ni vipi na ni kitu gani tunachokiamini.
- Mathayo 5:16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele za watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. 1 Petro 3:15 Basi mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.