JE, KIFO NI NINI?
Mhubiri 9:5 Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
6 Mapenzi yao na machukizo yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika lolote lililofanyika chini ya jua.
Kifo ni halia ambayo viumbe vyote vilivyohai lazima hatimaye vipitie ama kufikwa nayo. Ni hali ambayo kwayo kumbukumbu zote, mawazo na matendo mengine yote ya mwili husimama ama huacha kufanya kazi. Ni hali a,bayo husababisha mwili kuoza na kuyarudia mavumbi ya nchi.
- Mwanzo 3:19 Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katka hiyo ulitwaliwa; kwa maana, u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Wataki kifo kinapomjia mtu, anakuwa haishi tena hadi atakapokumbukwa katika siku ya ufufuo wa wafu. Atafufuliwa bila kujalisha kama ni mwema ama mbaya. wengine watafufuliwa kwa ufufuo wa uzima na wengine watafufuliwa kwa hukumu.
- Ayubu 19:25 Lakini mimi najua ya kuwa Mtetezi wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.
26 Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini pasipokuwa na mwili wangu utamwona
Mungu.
- 27 Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu!
- Yohana 5:28 Msisitaabu maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote walio makaburini wataisikia sauti yake.
- 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Wakati mwanadamu anapokufa pumzi yake humtoka na huacha kuishi. hufanyika kuwa ni mfu. hakuna roho inayoondoka, ni pumzi yake ile ya uzima tu. Nwanadamu ni mavumbi ya nchi na pumzi ya uzima. Kifo ni tendo la kutenganishwa kwa mavumbi na pumzi.
- Zaburi 146:4 Pummzi zake hutoka, hakuna wokovu kwake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.