JE MAUTI YA PILI NI NINI NA INAFANANISHWA NA NINI?
Ufunuo wa Yohana 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Je, hi mauti ya pili inayoongelewa ni nini hasa? Kabla hatujaelewa maana ya mauti ya pili, ni muhimu tukageukia kwanza nyuma na kujiuliza swali kuhusu nini hasa maana ya mauti ya pili? Kifo ni tendo la kukoma kwa matendo yote ya shughuli za mwili
- Zaburi 146:4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake hupotea;
Sasa, mauti ya pili ni kile kinachowatokea wenye dhambi baada ya kufufuliwa kwao toka kwa wafu kwa ajili ya kukabiliana na hukumu ya Mungu.
- Yohana 5:28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake,
- 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Waovu ama wenye dhambi watahukumiwa na kisha kutiwa kwenye mauti ya milele (yaani kifo). Watatupwa kwenye ziwa la moto na kuunguzwa kabisa. Watafanyika kuwa majivu yakanyagwayo na waongofu watakatifu.
- Zaburi 37:20 Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
- 35 Nimemuona mtu asiye haki mkali sana, Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.
- 36 Nikapita na kumbe! Hayuko, Nikamtafuta wala hakuonekana.
- Malaki 4:1 Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, wao wote watendao maovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa Majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
- 2 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.
- 3 Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini nyayo za miguu yenu, katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.
Waovu watateketezwa kabisa na kupotea usoni pa nchi na watakatifu watatembea juu ya mavumbi yao katika ufalme wa Mungu utakaofanyika hapa duniani