JE, ITAKUWA LINI?
2 Petro 3:7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata sikuya hukumu, nay a kuangamia kwao wanadamu wasiomtii Mungu.
- 10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi, katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
- 11 Bas, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafunuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
- 12 Mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
- 13 Lakini kama ilivyo ahadi yake, tunaitazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambamo haki yakaa ndani yake.
Tafadhali usizielewe vibaya aya hizo hapo juu. Ingwaje waovu wataunguzwa kabisa hapa duniani, dunia iliumbwa ili iweze kurithiwa milele. Mungu ataisafisha hii dunia kwa moto na kisha ataitakasa kwa kuifanya upya kwa misingi ile ambayo iliumbiwa kwayo toka mwanzo.
- Kumbukumbu la Torati 32:22 Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata nchi ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.
- Malaki 4:1 Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, wao wote watendao maovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa Majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
- 2 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.
- 3 Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini nyayo za miguu yenu, katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.
Baada ya kuangamiwa kwao waovu, Mungu atayafanya mambo yote kuwa mapya kwa kuifanya misingi ya dunia na kuanzisha utawala wake wa milele.
- Zaburi 104:1 Ee nafsi yangu, mhimidi BWANA. Wewe BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na adhama.
- 5 Uliiweka nchi chini ya misingi yake, Isitikisike milele.
- Ufunuo waYohana 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
- 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
- 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye amefanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake; Naye Mungu mwenyeweatakuwa pamoja nao.
Mhubiri 1:4 Kizazi huenda, kizazi huja, nayo dunia hudumu daima.
Isaya 45:18 Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.