JE, WAONGOVU WENYEHAKI WATAKUWA WAPI MILELE?
Jibu la swali lililopita linaanzia katika ahadi toka kwa Yehova kwa mtu aitwae Abraham.
- Mwanzo 17:1 Mwanzo 17:1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
- 2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.
- 3 Abramu akaanguka kifudifudi, Mungu akamwambia, akasema,
- 4 Mimi, agano langu nitalifanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi.
- 5 Wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.
- 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.
- 7 Agano langu litakuwa imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyako, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
- 8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
- Wagalatia 3:29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Yehova alimuahidi Abraham na uzao wake kwamba anawapa hii dunia kuwa milki yao ya milele. Kama wewe umeisha batizwa na kuzishika amri za Yesu Kristo hadi kufia mwisho wako, basi wewe ni wa uzao wa Abraham na kufanyika kuwa ni mrithi wa hii nchi milele
- Mhubiri 1:4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.
- Zaburi 104:5 Uliiweka nchi juu ya misingi yake, Isitikisike milele.
- Isaya 45:18 Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.
- Kumbukumbu la Torati 4:40 Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo BWANA, Mungu wako milele.
Watakatifu watairithi nchi ambayo imefanyizwa na kuchukua mahala pa Bustani ya Eden. Yehova ataishi na watu wake na kutawala hapa duniani milele.