JE, NANI ATAPASWA KUFA HII MAUTI YA PILI?
Ufunuo wa Yohana 20:12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu waka hukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
- 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
- 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto.
- 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa kwenye lile ziwa la moto.
Wale watakao hukumiwa kuingia kwenye hukumu mauti hii ya pili ni wale wote ambao hawakumkubali Yesu Kristo na kuzishika amri zake. Kama walikataa kuukubali ukweli wa kwamba alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zao na iwapo kama hawakubatizwa (tendo linalouonyesha ulimwengu toba yao), kwa hiyo, majina yao hayataonekana kwenye kitabu cha uzima. Watatupwa kwenye ziwa la moto kukifuatiwa na mauti na kuzimuni (kaburini) na hawataishi tena kwa kuwa watafanyika kuwa majivu yakanyagwayo na nyayo za miguu ya watakatifu.
- Malaki 4:1 Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, wao wote watendao maovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa Majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
- 2 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.
- 3 Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini nyayo za miguu yenu, katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.
Wakati hali hii ikitokea hakutakuweko na kifo tena na wale watakao salia wataishi maisha ya milele.
- Ufunuo wa Yohana 21:4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.