JE, KWA NINI ILIMPASA KRISTO KUFA?
Je, ni kwa nini mtu, safi na asiye na dhambi, afe kifo kama hiki cha kutisha msalabani?
- Waebrania 9:22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
- 23 Basi ilikuwa sharti nakala za mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.
- 24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yet;
- 25 Wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake;
- 26 Kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.
- 27 Na kama vile watu walivyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu:
- 28 Kadhalika Kristo naye, akiisha akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; katokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
Wakati mwanadamu alipofanya dhambi kwenye Bustani ya Eden, alilazimika kufa kama ni hukumu yake kwa kosa la kula tunda lililo katazwa. mauti hii ingekuwa ni ya milele kama Mungu asingeweka njia ya kuiepuka kwa kumtumwa Mwana wake mpendwa na wa pekee ili afe kwa ajili yetu. Damu ni uhai wa mwili, kwa hiyo basi, tendo la kumwaga damu husababisha kifo. Kwa hiyo, pasipo kumwagwa kwa damu hakuwezekani kuwepo kwa ondoleo (ama msamaha) wa dhambi. Ni Kristo tu aliye paswa kufa mara moja ili atuokoe wanadamu wote, sawa na vile ilivyotokea kwamba kwa kupitia dhambi za mtu mmoja mauti iliweza kumpata kila mwenye mwili.
- Warumi 5:12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
- 15 Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya watu wengi.
- 17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kila kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
- 19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.
Kristo alikufa ili atuokoe kutoka katika mauti ya milele iwapo tu kama tukiamwani kwa kiasi cha kuzishika amri zake hadi mwisho.