Je, Kwa nini Mwanadamu aliwekwa Duniani?
Kumbukumbu la Torati 30:19 Nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
20 Kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyo waapia baba zako, Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kuwa atawapa.
Mwanadamu aliwekwa hapa duniani na kupewa uhuru wa kuchagua kati ya kumtumikia Yehova au kumkataa. Mwanadamu alipewa uhuru wa kuchagua, ambao ulipelekea matokeo ya kuchagua uzima ama mauti. Mwanadamu hakupewa hiyari ya kuchagua kuumbwa kwake kwa hiyo hii ilifanyika kwa kupewa kwake uhuru wa kuchagua kuwepo kwake (yaani uzima) ama asiishi (yaani kifo, ambayo imefafanuliwa kwenye swali la pili). Mwanadamu alipewa ulimwengu wote na kila kiumbe chenye uhai ili viwe chini ya utawala ama uangalizi wake.
- Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanadamu alipewa kazi au jukumu la kuvitunza ama kuviangalia na kumtumikia Yehova peke yake na sio kuitumikia miungu mingine iwayo yote ile. Hivyo basi, hawakuweza kujishughulisha na aina iwayo yote ile ya mingu ya kipagani ama tamaa ziwazo zote zilizoko hapa duniani.
- Mhubiri 12:13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndivyo impasavyo mtu.
- 14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neon la siri, likiwa jema au likiwa baya.
- Kumbukumbu la Torati 8:19 Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya mtaangamia bila shaka.
- 1 Yohana 2:16 Maana kla kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tama ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.