MUNGU ni MMOJA
Imeandikwa ma James Herschel Lyda
Juni 27,2008
Kumbukumbu la Torati 6:4
inasema:- Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja,Marko 12:29 inasema:- Yesu akajibu,
Ya kwanza ndio hii, Sikiza, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;Yeye hayupo kwenye mfumo wa shirikisho la miungu miwili, wala wa mingu mitatu. Ila ni MUNGU MMOJA. Elimu ya Hisabati hutufundisha kwamba 1 haiwezi kuwa 2 wala kuwa 3 lakini inabakia kuwa ni ileile 1, na nambari hii 1 ni ya umoja na hubakia kuwa hivyohivyo siku zote na haiwezi kubadilika kuwa ni nambari ya uwingi ama ya jumuisho.haijafanywa kuwa ni nambari ya uwingi bali ni ya umoja tu siku zote.
1 Timotheo 2:5 inasema:- Kwa
sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;Wagalatia 3:20 inasema:- Bali aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja;
bali Mungu ni mmoja.Kuna MUNGU MMOJA tu na mpatanishi mmoja, ikimaanisha kuwa MUNGU NI MMOJA (neno "na" maana yake ni jumlisha) na mpatanishi mmoja, yaani 1+1=2. Kristo alitumwa awe mpatakishi wetu, au mwenye kusimama kati ya Mungu na mwanadamu. Alijifarakanisha na Mungu baada ya kumuasi kwake kwa kula tunda la mti uliokatazwa uliokuwa kwenye bustani na kumfanya Mungu asiwe na jingine la kumfanya mwanadamu ambaye sasa alikuwa ni sehemu ya dhambi yenyewe. Kwa hiyo alihitaji kuweko na mtu mwingine ili awe mpatanishi kati yake na mwanadamu. Mungu asingeweza kuwa mpatanishi kwa kuwa alikuwa amechukizwa na alilofanya huyu mwanadamu. Na mwanadamu asingeweza kuwa mpatanishi kwa kuwa alikuwa ndiye aliyefanya machukizo haya. Kwahiyo, alihitaji awepo mtu mwingine mwenye kusimama katikati yao, hivyo basi, Kristo, mtu aliye mkamilifu, ambaye alikuwa hajatenda dhambi yeyote.
Katika hizi Amri kumi za Mungu, tano za kwanza zinahusika na kuelezea kuhusu Mungu alivyo na taswira ya umoja na kuwa ni mmoja tu. Yeye ni Mungu mwenye wivu na hapendi kushirikisha aina yeyote ya utukufu wa kuabudiwa kwake na kiumbe kingi cho chote kile.
Kutoka 20:1 inasema:- Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu ya mbinguni, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usikisujudie wala kukitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu
7 Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase
Mungu ambaye anajua mambo yote hamtambui mungu mwingine yeyote na haipaswi kuwa na uwezekano wa aina yoyote wa kuwa na aina nyingine ya mungu hapa ulimwenguni.
Kumbukumbu la Torati 4:35 inasema:- Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa
BWANA ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye.Kumbukumbu la Torati 4:39 inasema:-Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa
BWANA ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine1 Wafalme 8:60
inasema:- Watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa BWANA ndiye Mungu; hakuna mwingine.Isaya 44:6 inasema:- BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na wamwisho;
zaidi yangu mimi hapana MunguIsaya 45:5
inasema:- Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua.Isaya 45:6 inasema:- ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi,
ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.Isaya 45:18 inasema:- Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu;
Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.Isaya 45:21 inasema:- Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, BWANA?
Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimiIsaya 45:22 inasema- Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana
mimi ni Mungu; hapana mwingineIsaya 46:9 inasema:- kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana
mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;Kutoka 3:6
inasema:- Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia MunguKutoka 3:14 inasema:-Mungu akamwambia Musa,
MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.(Hapa Mungu anasema kwamba
Mimi ndimi Mungu, na hasemi Mimi ndiye Mungu,yaani hasemi Mimi ndiye Mungu bali anatumia usemi huu wa ndimi akiashiria kwamba yeye alikuwa ni Mungu wa PEKEE aishiye hapa ulimwenguni)Zaburi 90:2 inasema:- Kabla haijazaliwa milima, wala hajaiumba dunia,
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.Zaburi 103:17 inasema:- Bali fadhili za BWANA zina wamchao
Tangu milele hata milele, Na haki yake ina wana wa wana.Zaburi 106:48 inasema:- Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli,
Tangu milele hata milele. Watu wote na waseme, Amina. Haleluya.Ni Mungu pekee ndiye aliyeishi na kuwepo tangu milele iliyopita na hadi ile milele ijayo. Huu ndio ukweli ambao imekuwa ni vigumu kukubalika na mwanadamu, kwamba Mungu amekuweko siku zote na anaishi tangu milele yote iliyopita na hata ile ijayo, na Mungu huyu hana mshirika katika uumngu wake.