Je, Mungu Yuko Wapi?

Na: James Herschel Lyda 8/25/2005

Je, Mungu yuko wapi na kwa nini anaruhusu mambo mabaya kutokea? Mnamo tarehe 20 Marchi, 1980 janga kubwa sana lilitokea ambalo lingewaamsha watu wa taifa hili likiwa kama onyo juu ya mambo mengine mengi mabaya yanayoweza kutokea. Mlima uitwao wa Mtakatifu Helens ulilipuka kwa jinsi ya tukio ambalo halijawahi kunukuliwa kutokea katika historia. Mlipuko huu uliua watu 57 na kuharibu au kuteketeza msitu wenye maili za mraba 230. Onyo hili lilipita bila kutiliwa maanani nasi kama taifa tuliendelea kumtomjali wala kumpa Mungu nafasi maishani mwetu.

Tulikuwa tunafundisha elimu ya mageuzi ya kimaumbile (evolution) badala ya uumbaji kwenye shule zetu lakini tulienda mbali na pabaya zaidi pale tulipopiga marufuku maombezi ya wazi kwenye shule zetu na kwenye makutaniko ya pamoja ya wazi. Sisi kama taifa hatukusikiliza maonyo ya Mungu.

Mambo ya walawi 26:14 Laikini msiponisikiza, wala hamtaki kuyafanya maagizo hayo yote;

15 nanyi mkizikataa amri zangu, na roho yenu ikichukia hukumu zangu, hata ikawa hamtaki kuyafanya maagizo yangu yote, bali mwalivunja agano langu;

16 mimi nami nitawatenda jambo hili; nitaamrisha uje juu yenu utisho, hata kifua kikuu na homa, zitakazoharibu macho yenu, na kuidhoofisha roho; nanyi mtapanda mbegu zenu bure, kwa kuwa adui zenu wataila.

17 Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambapo hapana awafukuzaye.

18 Tena ikiwa baada ya hayo hamtaki kunisikiza, ndipo nitaadhibu zaidi mara saba kwa ajili ya dhambi zenu.

19 Nami nitakivunja kiburi cha uwezo wenu; nami nitazifanya mbingu zenu kuwa kama chuma, na nchi yenu kuwa kama shaba;

20 na nguvu zenu mtazitumia bure; kwa kuwa nchi yenu haitazaa mazao yake, wala miti ya nchi haitazaa matunda yake.

21 Nanyi ikiwa mwaenenda kinyume changu, wala hamtaki kunisikiza; nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, kama dhambi zenu zilivyo.

Kwa hiyo Mungu alitupa maonyo tena mnamo tarehe 26 Februari, 1993 wakati watu sita walipouawa na wengine zaidi ya 1,000 walijeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu la Kitavu cha Biashara cha Kimataifa. Lakini je, tulimrudia Mungu baada ya hayo? Hapana! Nakala za Amri Kumi za Mungu zilikuwa zimeisha ondolewa kwenye majengo yote ya shughuli za umma na kwenye vyumba vyetu vya madarasa. Mungu alituonya tena tarehe 11 Septemba, 2001 kwa kuwaruhusu maadui zetu kuziteka ndege zetu wenyewe na kuruka nazo hadi kwenye majengo ya Kitovu cha Biashara cha Kimataifa na pia kwenye jingo la Wizara ya Ulinzi, the Pentagon na kuua takriban watu 2986. Hili ni tukio la mauaji makuu kabisa kupita yote katika historia ya nchi ya Marekani

Baada ya tukio hili la kuhusuriwa kwa Kitovu cha Biashara cha Kimataifa ndipo angalau gaadhi ya watu wetu walirudi makanisani na kulitumia neno la Mungu kwa mtazamo mzuri lakini hata hivyo hali hii ilidumu kwa kitambo tu. Kisha ikasahaulika na watu kurudi kwenye shughuli zao za kumuondoa Mungu atoke kabisa kwenye maisha yao. Hatujui kwamba tumejiingiza kwenye vita huko Iraq na Afghanistani ambayo hatuwezi kushindwa kwa kuwa Mungu hayupo pamoja nasi. Anawatumia adui zetu ili,kutuadhibu kwa ajili ya kutoamini kwetu na kwa kutozishika amri zake. Sisi kama taifa hatutaweza kamwe kupata ushindi kikamilifu tukiwa vitani hadi tutakapogeuka na kumrudia Mungu na kuzishika amri zake.

Kwa mara nyingine Mungu ameturudi tena kwa kosa la kutoamini kwetu na kwa kutozishika amri zake. Maafa ya vimbunga vya Katrina na Rita vimelipiga taifa hili kwenye "sehemu za mijini" ya nchi yetu na ilikuwa karibu kabisa iuhusuru New Orleans. Hili lilikuwa ni janga kubwa na lililogharimu sana kuliko yote kuwahi kutokea katika historia ya Marekani.

Ufunuo wa Yohana 18:1 Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wan chi wamezini naye, na wafanya biashara wan chi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.

6 Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni mara dufu.

7 Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.

8 Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyehukumu ni mwenye nguvu.

9 Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;

10 wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.

 

Je, Mungu anakuwa wapi wakati mambo haya yote yanapokuwa yanatikumba Marekani? Anakuwa ameketi kwenye kiti chake cha enzi kama afanyavyo siku zote na huku akituacha sisi tukiwa peke yetu, sawa na kama sisi tulivyomkataa yeye. Yeye hasababishi kutokea kwa mambo haya mabaya lakni anaruhusu yatokee na yawapate wana wa uasi na wasiozitubia dhambi zao. Anaruhusu haya yatokee ili kwamba sisi tujinyenyekeshe kwake na kurudi kwenye njia zake.

Tafadhali! Nawasihi watu wote wa taifa hili kuu letu tugeuke kutoka kwenye njia zetu mbaya na tumrudishe tena Mungu kwenye maisha yetu yote ya siri na yaonekanayo hadharani. Tunaweza kumuabudu Mungu hadharani bila ya kuvunja kanuni zinazotenganisha kanisa na serikali. Hebu basi na tumrudishe Mungu tena kwenye shule zetu na kwenye mahakama zetu. Hebu basi na tumrudishe Mungu kwenye maisha yetu kabla hatujachelewa.

REJEA KWENYE UKURASA MKUU